Upya wa Utenzi wa Mwana Kupona katika utenzi wa Howani Mwana Howani na Jawabu la Mwana Kupona
Ikisiri
Makala hii ililenga kuchunguza upya wa Utenzi wa Mwana Kupona katika utenzi wa Howani Mwana Howani na Jawabu la Mwana Kupona. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Bakhtin kuhusu lugha (1981) na Ufeministi wa Kiafrika iliyoasisiwa na Chioma (1980). Nadharia ya Bakhtin kuhusu lugha inashikilia kuwa lugha huwa na kani za aina mbili: nguvu za Kani Kitovu na Kani Pewa. Nguvu za Kani Kitovu zinafanya kazi kwa kuvuta vipengele vyote vya lugha na mbinu zake za ufasaha kuelekea katikati ili kutoa lugha moja iliyo sanifu au rasmi ambayo kila mmoja anaitumia. Nguvu hizo za Kani Kitovu zilikuwa kanuni zilozounganisha na kuleta kitu katikati. Nguvu za Kani Pewa zilijaribu kusukuma vipengele vya lugha kutoka katikati na kupelekea kuwa na wingi wa lugha au vijilugha. Kwa upande mwingine, Nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika iliasisiwa katika miaka ya 1980 na Chioma na Kuendelezwa na Ogundipe (1994), Nnaemeka (2003) miongoni mwa wengine. Nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika inafafanuliwa kama mapambano dhidi ya aina zote za dhuluma ili kupiga hatua katika kupata haki za wanawake. Jitihada hizi zinaweza kuwa za kijinsia, ubaguzi wa rangi, unyanyasaji wa kiuchumi kati ya dhuluma nyinginezo zinazolenga kumdhalilisha mwanamke (Bayu, 2019). Utafiti ulikuwa wa kimaelezo. Utafiti ulifanywa maktabani na nyanjani. Sampuli maktabani na nyajani iliteuliwa kimaksudi. Maktabani, mtafiti alisoma kwa kina matini iliyochapishwa kwa lengo la kupata data ya msingi. Nyanjani, mtafiti alifanya mahojiano na majadiliano na wanajamii walioteuliwa katika kukusanya data. Data kutoka katika tenzi zilizoteuliwa, maandishi yaliyohusu utafiti huu, data ya nyanjani zilichambuliwa kulingana na lengo la makala haya na mihimili ya nadharia kwa lengo la kuonyesha namna upya wa Mwana Kupona ulivyobainika katika utenzi wa Howani Mwana Howani na Jawabu la Mwana Kupona. Makala haya yalibainisha kuwa utenzi wa Howani Mwana Howani na Jawabu la Mwana Kupona zilisheheni upya kifani na kimaudhui katika mpito wa wakati.
Upakuaji
Marejeleo
Acholonu, C. O. (1995). Motherism: The Afrocentric Alternative to Feminism. Owerri: Afa Publications.
Allen, J. W. T. (1971). Tendi. Nairobi: Heinemann.
Bakhtin, M. (2001). Discourse in the Novel. Modern Literary Theory. 4th Edition. London: Routledge.
Bakhtin, M. M. (1981). The Dialogic Imagination: Four Essays by M. M. Bakhtin (Holquist, M. ed. Emerson, C. & Trans.).
Bayu, E. K. (2019). “A comparative analysis on the perspectives of African Feminism
Vs Western Feminism”: philosophical debate with their criticism and its implication for women’s rights in Ethiopia context. International Journal of Sociology and Anthropology Vol.11 (4), pp. 54-58, July-September 2019. http://www.academicjournals.org/IJSA
Beasley, C. (1999). What is Feminism? An Introduction to Feminist Theory. Available at: https://philpapers.org/rec/BEAWIF-2
Beja, S. K. & Mwinyifaki, A. (2013). ‘Iktibasi’ katika Tenzi za Mwanakupona na Al-Inkishafi. Kioo cha Lugha, 11(1), 30-46. Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Biersteker, A. (1991). “Language, Poetry and Power: A Reconstruction of ‘Utendi wa Mwana Kupona.’ In Harrow, K. W. (Ed.), ‘Faces of Islam in African Literature’. pp 37-58. London: James Currey.
Brandist, C. (2002). The Bakhtin Circle: Philosophy, Culture and Politics. London: Pluto Press.
Chioma, F. S. (1981). The Black Woman Cross-Culturally. Cambridge, Mass: Schenkman Publishers.
El-Maawy, A. A. A. (2011). Jawabu la Mwana Kupona. Dar es Saalam: Taasisi ya Taaluma za Kiswahili.
Ezeigbo, A. (2012). Snail-sense Feminism: Building on an Indigenous Model. Lagos:
Gibbe, A. G. (1995). Inkishafi: Uhakiki wa Kidayakronia. Tasnifu ya Uzamifu. Chuo Kikuu cha Moi. Eldoret. (Haijachapishwa).
Hirschkop, K. & Shepherd, D. (Eds.). (2001). Bakhtin and cultural theory. Oxford: Oxford University Press.
Holquist, M. (2002). Dialogism: Bakhtin and His World. London: Routledge.
https://btk.ppke.hu/uploads/articles/135505/file/introduction/satellite/literature_and_tradition.html retrieved on 27th March 2018. Islam International Publications.
Khatib, M. S. (1985). ‘Utenzi wa Mwana Kupona’ katika Mulika. Na. 17: 46-52. Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kolawole, M. M. (1997). Womanism and African Consciousness. Eritrea: Africa World Press.
Mbaabu, I. (1985). Utamaduni wa Waswahili. Nairobi: Kenya Publishing and Book Marketing Co. LTD.
Mbayi, L. A. (2009). Uhakiki wa Fani Katika Tenzi za Howani Mwana Howani na Mwana Kukuwa za Zaynab Himid Mohammed. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu Nairobi. (Haijachapishwa).
Mdee, J. S., Njogu, K. & Shafi, A. (2011). Kamusi ya Karne ya Ishirini na Moja. Nairobi: Longhorn.
Mohamed, F. A. (2016). Kuchunguza Mila na Desturi za Mwanamke wa Visiwani Pamoja na Fani katika Tenzi za Howani na Mwana Kukuwa. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. (Haijachapishwa).
Mohammed, Z. H. (1983) ‘Howani Mwana Howani-Kitunguu na Ubani’ katika Kiswahili Vol 50/2. 70-91.
Momanyi, C. (2007). ‘Patriachal Symbolic Order: The Syllables of Power as Accentuated in Waswahili Poetry.’ In The Journal of Pan African Studies, Vol. 1, No. 8. Pg. 12-32. California: California Institute of Pan African Studies
Mulokozi, M. M. (1999). Tenzi Tatu za Kale. Dar-es-salaam: TUKI.
Munyole, S. D. (2017). Usomaji na Ufasiri Sasa wa Utenzi wa Mwana Kupona. Chuo kikuu cha Kenyatta. Tasnifu ya Uzamili (Haijachapishwa).
Njozi, H. M. (1990). Utendi wa Mwana Kupona and Reception Aesthetics. Kiswahili,
, 55-67. Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Nana, W. (2010). “Feminism and Womanism”. A Concise Companion to Postcolonial Literature. 120-140. Wiley Online Library.
Nnaemeka, O. (2004). Nego-feminism: Theorizing, practicing, and pruning Africa’s way. Signs: Journal of women in culture and society, 29 (2), 357-385.
Nnaemeka, O. (2013). Foreword: Locating feminisms/feminists. Feminist local and global theory perspectives reader. New York: Routledge, 317-320.
Ogundipe, L. M. (1994). Re-creating Ourselves: African Women & Critical Transformations. Trenton, NJ: Africa World Press.
Ogunyemi, C. O. (1985). ‘Womanism: The Dynamics of the Contemporary Black
Female Novel in English’. Signs: Journal of Women in Culture and Society 11(1): 63-80.
Opara, C. (2005). ‘On the African Concept of Transcendence: Conflating Nature, Nurture and Creativity’. International Journal of Philosophy and Religion. 21(2): 189-200.
Stoeltje, B. (2015). Women, Gender and the Study of Africa. Oxford: New York.
Strobel, M. (1979). Muslim Women in Mombasa. 1890-1975. New Haven and London: Yale University Press.
Swaleh A. (1992). Maudhui Katika Utenzi wa Mwana Kupona. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa).
Timammy, R. na Swaleh, A. (2013). ‘A Thematic Analysis of Utendi wa Mwana Kupona: A Swahili Islamic Perspective’ In Journal of Education and Practice. Vol. 4, No.28: 60-72.
Tong, R. (2009). Feminist Thought: A More Comprehensive Introduction. Colorado.
University of Lagos.
Wamitila, K. W. (2003). Kichocheo cha fasihi: Simulizi na Andishi. Nairobi: Focus Publications.
Wamitila, K. W. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.
Wandera, S. P. (1996). “Usawiri wa Mwana Kupona Katika Ushairi wa Kiswahili: 1800-1900; Uhalisi au Ugandamizwaji? Tasnifu ya M. A; Chuo Kikuu cha Egerton. (Haijachapishwa).
Copyright (c) 2024 Gladys Kinara, Richard Makhanu Wafula, PhD, Pamela Muhadia Y. Ngugi, PhD

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.