Mfanano na Tofauti Baina ya Methali za Kiswahili na Kiarabu Katika Viwango vya Istilahi, Semantiki na Muktadha

  • Laabidi Abdelatiif Chuo Kikuu Huria Tanzania
Keywords: Istilahi, Kiarabu, Kiswahili, Methali, Muktadha, Utamaduni, Semantiki
Sambaza Makala:

Ikisiri

Lengo la makala hii ni kuchunguza kwa kulinganisha na kulinganua semantiki ya methali za Kiswahili na Kiarabu kwa kutumia vigezo vya maana ya kawaida na maana ya kimuktadha kulingana na nadharia ya Paul Grice. Jumla ya methali thelathini (30) za Kiswahili pamoja na methali thelathini (30) kifanani za Kiarabu zimetumika katika ulinganishaji na ulinganuaji. Kati ya methali hizo, methali kumi (10) zimeonesha mfanano katika nyanja ya maana ya kawaida ikiwamo na istilahi pamoja na maana ya kimuktadha. Wakati huo kuna methali kumi nyingine zinazoashiria utofauti wa maana ya kawaida ikiwamo na istilahi lakini kuna mfanano katika maana ya kimuktadha. Methali kumi (10) nyingine zinaashiria tofauti katika maana ya kiistilahi na maana ya kawaida lakini methali husika hutumika katika muktadha sawia. Hoja kuu katika makala hii ni kuthibitika kwa mwingiliano mkubwa baina ya methali za Kiswahili na Kiarabu japokuwa kuna tofauti kadhaa katika baadhi ya methali kupitia muundo wa kiistilahi na kimantiki, hata hivyo methali zote hutumika katika muktadha sawia. Matumizi ya methali zote zilizoshughulikiwa katika makala hii zimeashiria uhusiano mkubwa katika maana ya kimuktadha ambapo zimekuwa zikirejelea muktadha sawia kulingana na muktadha wa methali kifanani. Data ya makala hii ilikusanywa kupitia mahojiano pamoja na upitiaji nyaraka na matini. Sehemu kubwa ya data iliyokusanya inajumuisha methali za Kiswahili na Kiarabu pamoja na maana zake ambazo zimepatikana kupitia kamusi ya methali za Kiswahili. Kitaaluma, makala hii ni nyongeza muhimu katika ufahamu juu ya uhusiano wa Kiswahili na Kiarabu na inaendelea kuthibitisha uhusiano wa kiutamaduni wa muda mrefu baina ya utamaduni wa Mwarabu na Mswahili

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Arewa, E. O., & Dundes, A. (1964). Proverbs and the ethnography of speaking folklore. American Anthropologist, 66 (6), 70-85.

Barone, F. (2021). Knowledge is power: the anthropology of proverbs. Human Relations Area Files, Cultural Information for Education and Research, Yale University. Retrieved July, 14, 2024.

Coate, D. (2006). Lexical borrowing in Swahili from Arabic. Truman State University.

Coleman, B. E. (1971). A history of Swahili. The black scholar, 2(6), 13-25.

Karakacha, H. M., Zaja, O., Timammy, R., & Wamutiso, K. (2022). Proverb Usage and the Silencing of Women’s Voices: An Exploration of Swahili and Arabic Proverbs. Kioo cha Lugha, 19(1).

King'ei, K. G., & Ndalu, A. E. (1989). Kamusi ya methali za Kiswahili. East African Publishers.

Lubis, Syahron. (2019). “The Universality and Uniqueness of Proverb and Its Impact on Translation”. 10.2991/eltlt-18.2019.53.

Mtesigwa, G. K. (2013). Kuchunguza matumizi ya methali katika jamii ya wanyiramba. Chuo Kikuu Huria Tanzania. [Haijachapishwa]

Mwita, L. C. (2009). The Adaptation of Swahili Loanwords From Arabic: A Constraint-Based Analysis. Journal of Pan African Studies.

Ray, D. (2017). Defining the Swahili. In The Swahili World (pp. 67-80). Routledge.

Shembilu, M. M. S., (2015). Mapokezi ya kisemantiki ya nomino za mkopo katika Kiswahili: Mifano kutoka nomino zenye asili ya Kiingereza na Kiarabu. Kioo Cha Lugha. 13(1), 145 – 156.

Sini, I. & M. Soulaiman. (2010). Dictionary of Arabic Proverbs. Noor Book.

Tolmacheva, M. (1978). The Arabic influence on Swahili literature: a historian's view. Journal of African Studies, 5(2), 223.

Yankah, K. (1989). Proverbs: The aesthetics of traditional communication. Research in African Literatures, 20(3), 325-346.

Tarehe ya Uchapishaji
2 Septemba, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Abdelatiif, L. (2024). Mfanano na Tofauti Baina ya Methali za Kiswahili na Kiarabu Katika Viwango vya Istilahi, Semantiki na Muktadha. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 371-385. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2173