Usawiri wa Mhusika Mkinzani Katika Tamthilia Teule za Ebrahim Hussein: Kinjeketile (1969), Jogoo Kijijini (1976) na Arusi (1980)

  • Wilson Oluchili Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Richard Wafula Makhanu, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
##plugins.pubIds.doi.readerDisplayName##: https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2268
##share.article##:

Résumé

Makala hii imechunguza usawiri wa mhusika mkinzani katika tamthilia teule za Ebrahim Hussein; Kinjeketile (1969), Jogoo Kijijini (1976) na Arusi (1980). Swala la usawiri wa wahusika katika kazi za fasihi limeshughulikiwa na watafiti mbalimbali kwa mitazamo tofautitofauti. Usawiri wa wahusika wa kiume umetafitiwa na Kanwa (2022), nao unaohusu usawiri wa wahusika watoto umefanywa na Moige (2015). Aidha, Kitali (2011) naye ameshughulikia usawiri wa wahusika wa kike. Kutokana na uchunguzi wa watafiti, inabainika kuwa tafiti za awali kuhusu usawiri wa wahusika zimejikita kwenye wahusika wa kike, wa kiume, watoto, walemavu na wahusika kwa ujumla wasio wakinzani. Hivyo, panaibuka haja ya kumchunguza mhusika mkinzani na namna anavyosawiriwa katika tamthilia teule. Makala hii imeongozwa na nadharia ya Naratolojia ambayo iliwekewa msingi na Plato (1955) kisha ikandelezwa na Raglan (1936), Genette (1980) na Rimmon-Kennan (1983). Naratolojia inahusika na vipengele vya usimulizi vikiwemo; wakati, nafsi, nafasi, na wahusika. Kipengele cha wahusika ndicho nguzo iliyotumika katika utafiti huu kwani kinaelezea mbinu za usawiri wa wahusika na namna wanavyokuza maudhui. Data iliyotumika ilitolewa maktabani ambapo tamthilia teule, makala na vitabu vinavyohusiana na mada vilisomwa na kuchambuliwa kwa kina. Uwasilishaji wa matokeo umefanyika kw a njia ya maelezo yaliyoambatanishwa na dondoo mwafaka kutoka tamthilia teule. Matokeo yameonesha kuwa, katika tamthilia ya Kinjeketile na Jogoo Kijijini, mhusika mkinzani amechorwa kama mhusika asiyekuwepo kwenye jukwaa na ukinzani wake unabainika kupitia wanachokisema wahusika wengine na msimulizi kuhusu matendo yake. Mbinu alizosawiriwa nazo ni ya kuwatumia wahusika wengine, ya kinatiki, ya ulinganuzi na usambamba na ya kimaelezo. Kwa upande mwingine, mhusika mkinzani katika tamthilia ya Arusi amechorwa kama mhusika aliyepo kwenye jukwaa na ukinzani wake unabainika kupitia matendo na mazungumzo yake ya moja kwa moja na wahusika wengine jukwaani pamoja na wanachokisema wahusika wengine kumhusu. Mbinu alizosawiriwa nazo ni ya kinatiki na ya kuwatumia wahusika wengine

##plugins.generic.usageStats.downloads##

##plugins.generic.usageStats.noStats##

Références

Aristotle (1920). The Poetics. Oxford: Clarendon press.

BAKIZA (2010). Kamusi la Kiswahili Fasaha. Nairobi: Oxford University Press.

Chatman, S. (1978). Story and Discourse: Narrative Structure in Fiction and Film. Ithaca, New York: Cornell University Press.

Genette, G. (1980). Narrative Discourse. Ithaca: Cornell University Press.

Hussein, E. (1969). Kinjeketile. Nairobi: Oxford University Press.

Hussein, E. (1976). Jogoo Kijijini, Ngao ya Jadi. Nairobi: Oxford University Press.

Hussein, E. (1980). Arusi. Nairobi: Oxford University Press.

Kanwa, O. (2022). Usawiri wa Wahusika wa Kiume katika Riwaya za Kiswahili zilizoandikwa na Wanawake. Tasnifu ya Uzamifu, Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).

Keen, S. (2003). Narrative Form. London: Macmillan.

Kitali, H. N. (2011). Fani na Usawiri wa Wahusika wa Kike katika Tamthilia ya Pango na Mama ee. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Nairobi: University of Nairobi Publishers.

Margolin, U. (1983). Characterization in Narrative: Some Theoretical Prolegomena. Neophilogogus.

Moige, F. O. (2015). Usawiri wa Watoto Katika Riwaya za Kisasa za Kiswahili Zilizoandikwa na Muhamed Suleiman Muhamed na Euphrase Kezilahabi. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Egerton. (Haijachapishwa).

Mukobwa, J.N.M. (1985). Maendeleo ya Kimaudhui Katika Tamthilia Tano za Ebrahim N. Hussein. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa).

Njogu, K. na Chimera, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Okwena, S. (2019). Umahuluti wa Miundo katika Tamthilia Za Ebrahim Hussein. Tasnifu ya Uzamifu, Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).

Plato (1955). The Republic. Penguin Book Publishers.

Ponera, A. S (2014). Utangulizi wa Nadharia ya Fasihi Linganishi. Dar esalam: Karljamer Print Technology.

Propp, V. (1968). Morphology of the Folktale. University of Texas Press.

Rimmon – Kenan, S. (1983). Narrative Fiction. London: Methuen& Co. Ltd.

Rosefeldt, P. (2002). From Stage Interlude to Strange Snow: A Study of the Absent Character in Drama. A Journal of Evolutionary Psychology pp 117+. Institute for Evolutionary Psychology Publications.

TUKI. (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Nairobi: Oxford University Press.

Wamitila, K.W. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Msingi na Vipengele vyote. Nairobi Phoenix Publishers.

Wamitila, K.W. (2003). Kamusi ya Fasihi Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Books Publishers.

Publiée
15 octobre, 2024