Uchanganuzi wa Athari za Utamaduni Katika Tafsiri na Ukalimani wa Mahakama: Hali Halisi Kaunti ya Vihiga

  • Amola Cynthia Imbuga Chuo Kikuu cha Marafiki cha Kaimosi
  • Nabeta Sangili, PhD Chuo Kikuu cha Marafiki cha Kaimosi
  • Malenya Mary, PhD Chuo Kikuu cha Marafiki cha Kaimosi
##plugins.pubIds.doi.readerDisplayName##: https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2284
##share.article##:

Résumé

Utafiti huu umechunguza namna utamaduni unavyoathiri ukalimani na tafsiri katika mahakama ya kaunti ya Vihiga, ikizingatiwa kuwa kaunti hii imesheheni wingi wa lugha na mbari mbalimbali za Waluhya, hivyo, kuwepo kwa hitaji la ukalimani na tafsiri katika uendeshaji wa kesi mbalimbali mahakamani. Lahaja za Kitiriki na Kimaragoli zina utamaduni wao katika masuala mbalimbali kama vile: ndoa, tohara, mavazi, chakula, mawasiliano, na kadhalika. Utafiti huu umejikita katika utamaduni unaohusiana na mawasiliano pekee. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Isimujamii iliyoasisiwa na William Labov (1972) na nadharia ya Usawe iliyoasisiwa na Vinay na Darbelnet (1958). Utafiti huu ulitumia muundo wa Kifani. Mbinu ya kimaksudi ya usampulishaji ilitumiwa huku data ikikusanywa kwa njia ya uchunzaji, uchanganuzi nyaraka, na mahojiano kisha kuwakilishwa na kuchanganuliwa kidhamira. Utafiti huu ulifanywa nyanjani katika mahakama kuu mbili za kaunti ya Vihiga: mahakama ya sheria ya Vihiga na ya Hamisi. Ili kuhakikisha udhabiti na uhalali wa vifaa vya ukusanyaji data, utafiti awali ulifanywa katika Mahakama ya kisheria ya Kakamega. Mbinu ya upimaji wa uhalali wa maudhui katika vifaa vya utafiti ilitumika. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa, maneno ya kitamaduni ya lahaja za Kitiriki na Kimaragoli yanapodondoshwa wakati wa uhawilishaji, lugha pokezi inapokea hasara ya kutopata misamiati mipya. Wakalimani au watafsiri wanapolazimishwa kutamka maneno mwiko wananyimwa uwezo kuhifadhi uso wao katika mawasiliano ya kipragmatiki. Hivyo basi, matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwepo kwa athari za utamaduni wa lahaja ya Kitiriki na Kimaragoli katika tafsiri na ukalimani wa mahakama. Utafiti huu utaweza kuikuza taaluma ya tafsiri, ukalimani na isimu tekelezi kwa kutoa mchango wa jinsi ya kukalimani na kutafsiri diskosi mbalimbali

##plugins.generic.usageStats.downloads##

##plugins.generic.usageStats.noStats##

Références

Dictionaries, E. (2009). Encarta Encyclopaedia. Microsoft Student.

Gamal, M. Y. (2009). Court Interpreting. In Routledge Encyclopedia of Translation Studies (second edition ed., pp. 63- 67). https://shorturl.at/ahOQ9

Ihimud, M. (2023). Lost in Translation: Language Barriers to Accessing Justice in the Amercan Court System.UIC Law Review, 56(4). https://repository.law.uic.edu/lawreview

Kaschula, H., & Andre, M. (2022). Communicating across cultures in South African law courts. Towards an Information Technology Solution Department of African Languages. https://shorturl.at/bvxZ4

Labov, W. (1972). Some Principles of Linguistics Methodology. Language in Society, 1(1), 97-120. https://shorturl.at/6mVDh

Leal, K. (2018). Legal Translation and Court Interpreting in Laredo. Doctorial dessertation ,Texas A & M International University, Laredo. Retrieved from https://shorturl.at/kGIV8

Lebese, S. (2011). A Pilot Study on the Undefined Role of Court Interpreters in South Africa. Southern African Linguistics and Applied Language Studies, 29(3), 343-357. https://shorturl.at/blpyE

Machani, J. (2017). The Challenges of Equivalence in Language Structure in the Interpretation of Discourses of Actors in Court Proceedings in Kericho Law Courts. Doctorial dissertation,University of Kabianga. https://shorturl.at/arzKW

Marube, T. (2011, October 17). Standard Digital. Court Interpretation needs "revamp". Retrieved from https://shourt.at/tFR23

Mulwa, E., & Madule, D. R. (2023). Justice through Interpreting in Courts. A Case of Machokos Courts in Machakos, Kenya. Journal of Research Innovation and Implication in Education, 7(4), 821-833.

Mwansoko, H. J., Mekacha, R., Masoko, D., & Mtesigwa, P. (2013). Kitangulizi cha Tafsiri: Nadharia na Mbinu. Dar es Salaam: TUKI Publisher

Newmark, P. (1988). A Textbook on Translation. Prentice-Hall,Europe: HemelHempstead.

Nida, E., & Taber, C. R. (1969). The Theory and Practice of Translation. London: Prentice Hall.

Nida, E. (1979). Translating Means Communicating:A sociolinguistic theory of translation. The Bible Translator, 30(3), 43-50https://shorturl.at/dlpCD

Owiti, B. (2014). Meaning Loss in Interpretation:A Judgement Ruling in Nyando Magistrate’s Court, Kenya. http://repository.must.ac.ke/handle/12345678

Panou, D. (2013). Equivalence in Translation Theories: A Critical Evaluation. Theory and Practice in Language Studies, 3(1).https://shorturl.at/flxNX

Sangili, N. K. (2019). Udumishaji wa Lugha ya Kimaragoli katika Eneobunge la Uriri, Kenya. Rongo University, Doctorial dissertation.

Santos, E. (2022). Sociolinguistic as a Crucial Factor in Translation and Analysis of Text A Systematic Review. Internationa Journal of Translation and Interpretation Studies, 2(1), 91-97. https://rb.gy/iwhqe

The Constitution of Kenya. (2010). Nairobi. Kenya: Kenya National Law Reporting.

Tineke, J. (2022). Culture and the Court Interpreter:An Examination of Current Literature on Dealing with Potential Intercultural Miscommunication in the Court. New Zealand Journal of Translation Studies. https://shorturl.at/huX45

TUKI. (2000). A Standard English-SwahiliDictionary. Nairobi, Kenya: Printing Services Ltd.

Vinay, J. P., & Darbelnet, J. (1958). Stylistique Comparee du Francais et de l'Anglais: Methode de Traduction. Paris Didier: Amsterdam/Philadelphia: Benjamins.

Wang, D. Y. (2014). Examining the Challenges of Legal Interpreters in New Zealand Courtroom Setting. Doctorial dissertation,Auckland University of Technology. https://shorturl.at/CIL26

Wangia, J. (2014). Tense,Aspect and Case in Bantu and Signifance in Translation:Case of Kimaragoli Bble. International Journal of English Language and Translation Studies (2), 138-158.

Wanjala, F. S. (2011). Misingi ya Ukalimani na Tafsiri Kwa Shule, Vyuo na Ndaki. Mwanza, Tanzania: Serengeti Educational Publishers (T)

Publiée
8 octobre, 2024