Udhihirikaji wa Viambajengo Katizwa Katika Lugha ya Kiswahili

  • Priscah Katunge Lucas Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Leonard Chacha Mwita, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Viambajengo Katizwa, Sentensi Katizwa, Virai Katizwa
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inachunguza udhihirikaji wa viambajengo katizwa katika Kiswahili. Viambajengo katizwa ni elementi za neno au kishazi ambazo hazipatikani katika usanjari mmoja kwa sababu elementi kutoka mofu au kirai kingine zimeingilia kati (Reinholtz, 1999). Hili hutokea wakati mofu kadhaa za kiambajengo kimoja zimetengwa au maneno kadhaa ya kirai kimoja yametengwa.  Kwa mfano: “Rais alizungumza, bila shaka, juu ya siasa.” Katika sentensi hii, kitenzi na kielezi chake vilitengwa na taarifa nyingine. Nadharia ya Sarufi Miundo Virai Katizwa iliyozungumziwa na Harman (1963) iliongoza utafiti huu. Data ya makala hii ilikusanywa nyanjani ambapo wataalamu wa lugha ya Kiswahili walihojiwa kuhusu usahihi wa sentensi katizwa na hata kusaidia kuzalisha zingine. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika katika uteuzi wa sampuli. Data ya utafiti huu ilibaini aina mbili kuu za virai katizwa. Ilibainika kuwa viambajengo katizwa husababishwa na ukanushi wa baadhi ya vitenzi, ukanushi maradufu, njeo vishazi tegemezi na vishazi viongezi. Tafiti zingine zinaweza kufanywa kuhusu udhihirikaji wa viambajengo katizwa katika aina nyingine ya kirai kama vile kirai kihusishi au kirai kivumishi katika lugha ya Kiswahili au lugha nyingine

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Bloomfield, L. (1933). Language. New York: Holt, Rinehart &Winston.

Chomsky, N. (1965). Aspects of the Theory of Syntax. MA: MIT Press.

Habwe, J. & Karanja, P. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers.

Harman, G. (1963). Generative Grammars without Transformaton Rules: A Defense of Phrase Structure. Language 39, pg. 597-626.

Lincoln, Y. S., & Guba, E. G. (1985). Naturalistic inquiry. Newbury Park, CA: Sage.

Manaster-Ramer, A. & Kac, M. B. (1990). The Concept of Phrase Structure. Linguistics and Philosophy, Jun., 1990, Vol. 13, No. 3 (Jun., 1990), pp. 325- 362. https://www.jstor.org/stable/25001390

Massamba, D. P. (2004). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. TUKI: Dar es Salaam.

Milroy, A. L. (1987). Observing and Analysing Natural Languages. Oxford: Bas Blackwell Ltd.

Poole, G. (2002). Syntactic Theory. New York: Palgrave.

Reinholtz, C. (1999). On Characterization of Discontinuous Constituents: Evidence from Swampy Cree. International Journal of American Lingustics, 65(2), pg 201-227. https://www.jstor.org/stable.

Rubanza, C. (2003). Basic Reading. Dar es Salaam: Macmillan Aidan Ltd.

Tarehe ya Uchapishaji
31 Oktoba, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Lucas, P., & Mwita, L. (2024). Udhihirikaji wa Viambajengo Katizwa Katika Lugha ya Kiswahili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 514-524. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2355

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.

1 2 > >>