Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Ikisiri
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni kitabu mojawapo kikongwe cha fasihi ambacho huwasilisha taswira changamano kuhusu binadamu. Katika kitabu cha Mwanzo 1:26-27, lugha inayotumiwa katika Biblia Takatifu inatuchorea taswira kuhusu hadhi ya mwanamke na mwanamume kuinuliwa kwa pamoja kulingana na mpango asili uliopendekezwa na Mungu. Hata hivyo, kupitia hiyo Biblia Takatifu, tunakumbana na taswira changamano zinazowasilishwa kuhusu mwanamke. Hili huwezeshwa kupitia lugha. Ikumbukwe kuwa lugha inayotumika katika Biblia Takatifu ina athari kubwa katika uhalisia wa kijamii, ikizingatiwa kuwa idadi ya wakristo wanaozingatia mafunzo ya Biblia Takatifu ni wengi (bilioni 2.4). Utafiti huu unachanganua vipengele vya sanaa vinavyojenga taswira ya mwanamke katika vitabu teule vya Biblia Takatifu. Madhumuni yaliyoshughulikiwa ni Kwanza, kuchanganua maumbo ya fasihi yanayojenga taswira ya mwanamke katika vitabu teule vya Biblia Takatifu na pili, kudhihirisha maudhui yanayojitokeza katika maumbo yanayojenga taswira ya mwanamke katika vitabu teule vya Biblia Takatifu. Utafiti huu ulijikita tu kwa maumbo ya fasihi na maudhui yanayowasilishwa katika taswira ya mwanamke katika vitabu teule vya Biblia Takatifu, toleo la 2013. Utafiti ulizingatia mseto wa nadharia; nadharia ya Umuundo mpya iliyorejelewa na Crick (2016), nadharia ya Umaumbo ambayo ilirejelewa na MaryAnne (1999), na kiunzi cha nadharia ya Ufeministi kwa mujibu wa Wamitila (2003). Muundo wa kiuchanganuzi ulizingatiwa. Mbinu ya uchunzaji ilitumiwa kuufanikisha huu utafiti. Makala yanayodhihirisha taswira ya mwanamke katika Biblia Takatifu ndiyo yaliyodondolewa. Orodhahakiki ilitumiwa kudondoa data kutoka kwenye Biblia Takatifu ili kupata sampuli zifaazo za maumbo na maudhui. Usampulishaji dhamirifu ulitumiwa kwa kuongozwa na madhumuni ya utafiti huu. Utafiti umebaini kuwa maumbo ya fasihi yanayojenga taswira ya mwanamke katika Biblia Takatifu yanaibua maudhui hai, aidha yanayoishi katika jamii, hivyo, kuna uwezekano kuwa lugha katika Biblia Takatifu imeathiri jamii halisi kwa namna hasi na chanya. Utafiti unatarajiwa kuwafahamisha wanajamii na umma kwa jumla kuwa nafasi ya mwanamke ni muhimu katika kuendeleza jamii na utaweka wazi namna lugha katika Biblia Takatifu inavyoathiri mtazamo wa jamii halisi kumhusu mwanamke
Upakuaji
Marejeleo
Agiso, Y. (2017). Mwingiliano Matini wa Maumbo ya fasihi simulizi ya kiafrika na matini teule za Biblia, Tasnifu ya uzamili, chuo cha Maseno.
Angelou, M. (2020). Phenomenal Women, Literary Devices. https;//litararydevices.net
Crick, N. (2016). The Oxford Encyclopedia Of Communication And Critical Cultural Studies: United Kingdom.
Euphrase, K. (1974), Kichomi: Lusaka: Heinemann.
Fowler, R. (1975), Style And Structure In Literature. Basil Blackwell. Penguine.
Gicuku, M. (2012), Usawiri wa maudhui ya ndoa katika Ushairi wa Euphrase Kezilahabi na kithaka wa Mberia. (Tasnifu ya Uzamili). Chuo kikuu cha Kenyatta, Nairobi.
Kamusi Ya Aina Ya Jinsia na Jinsia, (2010)
MaryAnn, C. (1999). Problematizing Formalism. A Double Cross of Genre Boundaries “College” Composition And Communication. 51:1 Sept 1999. 89 – 95
Masebo, J.A & Nyangwine, N. (2007). Nadharia Ya Fasihi. Dar es Salaam: Nyambari Nyangwine.
Merolla, D. (2017). Gender And Community in The Oral And in the Written Thesis at Leiden University. Algeria.
Murungi, G. K. (2013). Mtindo Unavyoendelezwa Kwa Maudhui Katika Natala. Tasnifu Ya Uzamili, Chuo Kikuu Cha Nairobi.
Mwangi, D.K. (2005). Uhakiki wa fani katika tamthilia za K. W. Wamitila. Tasnifu Ya Uzamili; Chuo Kikuu Cha Nairobi.
Nguta (2011) Fani na Usawiri wa wahusika wa kike katika tamthilia ya pango na Mama ee. Tasnifu ya Uzamili; chuo kikuu cha Nairobi.
Saro, J. (2017) Kuchunguza Usawiri Wa Mwanamke Katika Riwaya. Mfano wa Riwaya Ya Utengano . Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania.
Senkoro, F. E. M. K. (1982) “Silie Mwana Silie. Children’s Lyllabies from Tanzania, Paper read at the Annual Conference of the African Literature Association, Howard University, Washington D. C.
Sinzore S. (2019), Taswira Ya Mwanamke Kiongozi Katika Tamthilia Teule Za Kiswahili Tangia Mwaka 2000 Hadi 2016.Tasnifu Ya Uzamili; Chuo Kikuu Cha Maseno.
Shonko, D (2012), Kiswahili kwa Ajili Ya kusafisha
Timaywa, F. (2017), Kuchunguza Ujinsia Na Matumizi Ya Lugha Katika Methali Za Wakurya. Tasnifu Ya Uzamili. Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania.
Wamitila. K.W. (2003). Kamusi Ya Fasihi, Istilahi Na Nadharia: Focus Publications Ltd. Nairobi.
Wamitila, K.W.(2003). Pango. Nairobi:Focus Publishers.
Wamitila. K.W.(2003). Kichocheo Cha Fasihi: Simulizi na Andishi. Nairobi: Focus Publications.
Wamitila. K.W.(2003b) Kamusi Ya Fasihi, Istilahi na Nadharia: Nairobi. Focus Publications Limited.
Wanjiku, M. (1993),“Taswira ya wanawake katika Simulizi za Gikuyu Tasnifu ya Chuo Kikuu Cha Nairobi.
Copyright (c) 2024 Aglen Angwehe, Beverlyne Asiko Ambuyo, PhD, Benard Odoyo Okal, PhD

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.