Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
الملخص
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika ngazi ya kitaifa nchini Kenya ambapo mfumo wa elimu wa 8-4-4 unaondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na mtaala wa umilisi (CBC). Mabadiliko haya yamejikita katika elimu ya msingi, kuanzia kiwango cha chekechea, shule za upili hadi kwenye vyuo vinavyotoa elimu ya kiufundi kote nchini. Kwa sasa, mabadiliko katika mtaala wa kitaifa hayajaathiri vyuo vikuu kunakotolewa elimu ya juu. Hata hivyo, wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu huandaliwa kupitia kwa mafunzo ya shule za upili. Hivyo basi mabadiliko yoyote yanayotokea katika elimu ya msingi lazima yataathiri programu za mafunzo yanayotolewa katika vyuo vikuu. Makala haya yataangazia kipengele cha tathmini katika vyuo vikuu kwa kuzingatia mabadiliko katika mfumo wa elimu uliopo na vigezo vinavyoelekeza tathmini katika mfumo wa elimu wa umilisi. Mabadiliko katika tathmini katika mfumo wa elimu wa umilisi yanaashiria kuwepo haja ya kufanya mabadiliko sawia ya tathmini katika mafunzo ya elimu ya juu katika vyuo vikuu. Hali hii inatokea kuwa hivi kwa kuwa wanafunzi wanapojiunga na vyuo vikuu watakuwa wamezoeshwa tathmini ya shule za upili ambayo hufanyika katika kila hatua ya ujifunzaji mafunzo yanapoendelea tofauti na illivyokuwa awali ambapo tathmini ilifanyika mara moja mwishoni baada ya kipindi maalumu cha mafunzo (mwishoni mwa miaka minane katika shule za msingi na miaka minne katika shule za upili). Swali hapa ni je, tathmini ya awali iliyozoeleka na ambayo ilifanyika baada ya kipindi maalumu bado itafaa? Bado itafikia malengo yaliyopo ya elimu? Kufikia sasa, hakuna mwelekeo wowote ambao umetolewa kuhusiana na hili. Hali hii inapelekea kuwepo haja ya kubuni sera itakayotoa mwelekeo kuhusu vigezo vinavyofaa kuzingatiwa katika kubadili tathmini katika vyuo vikuu ili iendane na mabadiliko yanayoendelea kutokea katika mfumo wa elimu uliopo. Mabadiliko katika tathmini vyuoni yanaweza kufanyika kwa kulinganisha na kulinganua tathmini iliyokuwepo awali na iliyopo hivi sasa katika elimu ya msingi na vyuo vikuu. Makala haya yamechanganua changamoto zinazotokana na hiyo mifumo miwili ya tathmini na kuangazia namna ambavyo aina zote mbili za tathmini humwathiri mwanafunzi ambaye ndiye mwathiriwa mkuu. Makala haya yamelenga kuwezesha vyuo vikuu kutambua mielekeo na mitazamo ambayo wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga navyo huingia nayo vyuoni kutokana na namna wanavyotathminiwa wanapopokea elimu ya msingi. Makala haya yametokana na uchambuzi na mapitio ya maandishi yaliyopo tayari kuhusu mifumo hii miwili ya elimu pamoja na maoni ya wataalamu wa masuala ya mitaala. Maandishi haya yalipatikana maktabani na mitandaoni.
التنزيلات
المراجع
Kabita, D.N. and Ji, L. (2017). The why, what and how of competency-based curriculum reforms: The Kenyan experience. Process reflection no 11 on current and critical issues in curriculum, learning and assessment, UNESCO/IBE.
Kariya, T. (2000). The distance between educational reforms and education in the classroom. Child Research Net. URL:http//www.childresearch.net
Kaviti, L. (2018). The New Curriculum of Education in Kenya: A Linguistic and Education Paradgm Shift.IOSR-JHSS. Juzuu 23, Toleo la 2
Education at a Glance 2013, “Organisation for Economic Cooperation & Develoment. September 2013.http//www.oecd.org./edu/eag2013.htm
Ogutu, D.M. (2017).Education System Change: Perspectives from Kenya. Meaningfu education in times of uncertainity. Acollection of essays from Centre for Universal Education and top thought leaders in the fields of learning, innovation, and technology. Secretariat East Africa Community, (2007). https://kicd.ac.ke/wp content/uploads/2017/10/CURRICULUMFRAMEWORK.pdf
Secretariat East African Communuty, (2012). https://kicd.ac.ke/curriculum-reform/need-assessment-reports-for-cbc/
Yorke, M. (2003). Formative assessment in higher education: Moves towards theory and the enhancement of pedagogic practice. Higher education, 45 (4), uk.477-501.
الحقوق الفكرية (c) 2025 Jackline Osagi Mwanzi

هذا العمل مرخص حسب الرخصة Creative Commons Attribution 4.0 International License.