Utafiti wa Lahaja Kupitia Macho ya Jamii: Matumizi ya Mtazamo Tambuzi wa Elimu Lahaja Katika Kaunti ya Lamu
Ikisiri
Utafiti huu unachunguza uainishaji wa mipaka ya lahaja za Kiswahili zinazozungumzwa katika Kaunti ya Lamu, Kenya, kwa kutumia nadharia ya Mtazamo Tambuzi wa Elimu Lahaja (Preston, 1989). Tofauti na tafiti za awali zilizozingatia vipengele vya kimuundo vya lugha, utafiti huu umejikita katika maoni, mitazamo, uelewa na hisia za wasemaji wazawa kama vigezo halali vya kutambua na kuainisha lahaja. Kwa kutumia mbinu ya uchoraji wa ramani za mikono, sauti zilizorekodiwa, na mijadala ya vikundi, washiriki waliainisha maeneo ya lahaja kwa msingi wa tajriba zao binafsi. Data hiyo ilichakatwa kwa kutumia teknolojia ya GIS (QGIS na ArcGIS) kwa njia ya Kernel Density Estimation (KDE). Matokeo yameonyesha kuwepo kwa makundi makuu manne ya lahaja: Kiamu, Kipate, Kisiu na Kitikuu, huku Kishela na Kimatondoni zikiwa kwenye hatari ya kufifia kutokana na ushawishi wa Kiamu. Aidha, vipengele vya kifonolojia, kimofolojia na kisintaksia vilijitokeza kuwa msingi wa utambuzi wa tofauti hizo. Imebainika kuwa asili ya mzungumzaji, uzoefu wa lugha, na uhusiano wa kijamii ni vigezo muhimu vinavyoathiri namna wanavyotambua na kuchora mipaka ya lahaja. Utafiti huu unatoa mchango mpya kwa taaluma ya isimu-jamii na lahaja kwa kusisitiza umuhimu wa data tambuzi kutoka kwa jamii, na hivyo kupanua upeo wa utafiti wa lugha za Kiafrika kutoka katika mtazamo wa jamii kuelekea usomi wa kitaaluma
Upakuaji
Marejeleo
Abdalla, M. (1998). Kiswahili na maendeleo ya jamii ya Waswahili. Nairobi: Longhorn Publishers.
Bakari, M. (1985). The state and the academic achievement of Swahili in Kenya. University of Nairobi.
Boughton, R. W. (2006). Perceptual dialectology and folk linguistics. In L. L. Cummings (Ed.), Handbook of Pragmatics (pp. 1–20). Elsevier.
Chiragdin, S. H., & Mnyapala, A. S. (1977). Historia ya Kiswahili. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.
Coupland, N. (1988). “What do you mean?”: The elaboration of context in sociolinguistic explanation. In N. Coupland (Ed.), Styles of Discourse (pp. 11–30). Routledge.
Giles, H., & Niedzielski, N. A. (1998). Italian is beautiful, German is ugly. Language Myths, 85–93.
Hinnebusch, T. J. (1996). Dialects and variation in Swahili. In A. Nurmilaakso (Ed.), Topics in African Linguistics (pp. 47–68). Köln: Rüdiger Köppe Verlag.
Karanja, P. N. (2012). Swahili dialectology in the light of recent research. Nairobi: Kenya Literature Bureau.
Khalid, A. (1977). The Swahili dialects: A lexicostatistical classification. Dar es Salaam: University Press.
Kihara, R. W. (2011). Mienendo ya matumizi ya Kiswahili katika vyombo vya habari nchini Kenya. Nairobi: Phoenix Publishers.
Massamba, D. P. B. (2004). Studies in Bantu phonology: A tonal approach. Dar es Salaam: Institute of Kiswahili Research.
Mwinyi, A. (2004). Lugha ya Kipate na changamoto za uainishaji wa lahaja. Nairobi: University of Nairobi Press.
Nabhany, A. H. (1995). The Swahili dialects: A historical perspective. Nairobi: Swahili Centre for Linguistic Research.
Niedzielski, N. A., & Preston, D. R. (2000). Folk linguistics. Berlin: Mouton de Gruyter.
Nurse, D. (1979). Classification of the dialects of the north-east coast Bantu. African Language Studies, 16, 101–118.
Polomé, E. C. (1967). Swahili language handbook. Washington, D.C.: Center for Applied Linguistics.
Preston, D. R. (1999). Hand-drawn maps as a tool in linguistic research. In D. R. Preston (Ed.), Handbook of Perceptual Dialectology, Vol. 1 (pp. 275–292). Amsterdam: John Benjamins.
--------------- (1989). Perceptual dialectology: Nonlinguists’ views of areal linguistics. Dordrecht: Foris Publications.
Stigand, C. H. (1915). Dialect in Swahili: A grammar of dialectic changes in the Swahili language. Cambridge: Cambridge University Press.
Copyright (c) 2025 Judy Wangari Onyancha, Rayya Timammy, Mungai Mutonya

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.