Uangavu wa Maana kama Nyenzo ya Ujalizaji katika Lugha ya Kiswahili

  • Amulike Abraham Mwampamba Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
  • Lohay Marko Labiswai Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Keywords: Sintaksia, Kijalizo, Uangavu wa Maana
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yanahusu uangavu wa maana kama nyenzo ya ujalizaji katika lugha ya Kiswahili. Lengo la makala haya ni kuonesha kuwa ujalizaji huwa wa lazima ili kukidhi uangavu wa maana na si kukidhi miundo pekee. Data za makala haya zimekusanywa kwa njia ya usomaji makini, kuchambuliwa kwa nadharia ya Uchambuzi wa Maudhui na kuwasilishwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Aidha, wataalamu wengi wanakieleza kijalizo kama kipashio mojawapo katika sentensi. Hata hivyo hawabainishi wazi ulazima wa kijalizo katika sentensi huukiliwa na nini. Baadhi wanataja tu kuwa kijalizo ni cha lazima katika muundo wa sentensi. Miongoni mwao ni Massamba (2004); Habwe na Karanja (2004); Koech (2013); Matei (2017); Philipo na Kuyenga (2017) na Mtego (2022). Makala yameonesha jinsi uangavu wa maana unavyokifanya kijalizo kuwa cha lazima katika sentensi za Kiswahili. Makala yamedhihirisha kuwa kijalizo huwa cha lazima si tu kukidhi miundo ya sahihi bali pia kukidhi uangavu wa maana katika sentensi za lugha. Matokeo ya makala haya yameonesha kuwa ujalizaji katika tungo si jambo la hiari bali ni hitaji la lazima. Ulazima wa ujalizaji katika tungo hutokana na ukweli kwamba ili tungo iwe na uangavu lazima pawepo ujalizaji. Kwa hiyo, mwandishi anapendekeza kwamba ujalizaji katika tungo usifanyike ili tu kukamilisha muundo wa tungo pekee bali ufanyike ili kuleta uangavu wa maana katika tungo. Kwa kuwa lengo la lugha ni kukidhi mwasiliano, tungo zenye uangavu utokanao na ujalizaji ndizo zenye uwezo wa kufikia hitajio hilo

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Al-Luhaibi, K. E. A. (2024). Subject and object in complement control in language. The Islamic University College Journal, 57(2), 79-86.

Bavuai, I. A. (2017). Muundo wa kirai nomino katika lahaja ya Kimakunduchi. (Tasinifu ya uzamili wa Kiswahili). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Betti, J. M. (2013). Complement and complementation. Thi Qar University.

Betti, J. M. & Igaab, K. Z. (2021). Complement and complementation. University of Thi-Qar.

Buliekova, A. (2020). Word order variation of some object complement. Univerzita Karlova.

Carter, R. A. & Mc Carthy, M. J. (2006). Cambridge Grammar of English. Cambridge University Press.

Crystal, D. (2008). A dictionary of linguistics and phonetics (6th ed.). Blackwell Publishing.

Habwe, J. & Karanja, P. (2004). Misingi ya sarufi ya Kiswahili. Phoenix Publishers.

Haji, V. A. (2018). Kutathmini mbinu za usawiri wa wahusika katika riwaya ya dunia uwanja wa fujo na asali chungu:Utafiti linganishi. [Tasinifu ya shahada ya uzamili]. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Halliday, M. A. K. (2014). Introducing functional grammar (3rd ed.). Routledge.

Hassan, F. (2021). Mikabala ya uchanganuzi wa viambajengo vya sentensi na istilahi zinazotumika: mifano kutoka lugha ya Kiswahili. MULIKA 40(2), 1-22.

Hassan, F. & Kahigi, K. (2022). Uangavu wa kisemantiki kama nyenzo ya ufundishaji na ujifunzaji wa msamiati wa Kiswahili kwa wageni. Mifano ya nomino ambatani na nyambuzi. Katika Mtesigwa. P na Dure. E. (wah.). Kiswahili katika anga za kimataifa. TATAKI na BAKITA, 91-124.

Hudson, R. R. (2016). Uangavu wa kimofosemantiki katika nomino na vitenzi vya Kiswahili sanifu. (Tasinifu ya Shahada ya uzamili). TATAKI.

Jilala, H. (2024). Tathmini ya matumizi ya akili unde kama nyenzo ya kutafsiri matini za Kiingereza kwenda Kiswahili. Journal of Kiswahili and African Languages, 2(2), 1-13.

Kanichi, N. M. (2018). Uchanganuzi wa Kirai cha Kibantu-Mtazamo wa X-baa. Mfano: Kutoka Kirai nomino na kitenzi cha Kinyakyusa. (Tasinifu ya shahada ya uzamili, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, haijachapishwa).

Kipacha, A. (2007). Utangulizi wa lugha na isimu. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Koech, L. (2013). Sintaksia ya kijalizo cha Kiswahili sanifu: Mtazamo wa x baa. (Tasinifu ya uzamili, haijachapishwa). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Khamis, A. M. (2008). Maendeleo ya uhusika. TUKI.

Krippendorff, K. (2004). Content analysis and introduction to its methodology. Sage Publications.

Ma, W. (2014). Corpus based analysis of semantic transparency between high frequent English and Chinese compounds. Academy Publisher.

Massamba, D. P. B. (2004). Kamusi ya isimu na falsafa ya lugha. TUKI.

Massamba, D. P. B. na wenzake (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu. TUKI.

Matei, A. K. (2017). Darubini ya sarufi: ufafanuzi kamili wa sarufi ya Kiswahili.

Matinde, S. R. (2012). Dafina ya lugha: isimu na nadharia. Serengeti Educational Publishers (T) Ltd.

Masota, K. E. (2016). Utohozi wa msamiati kutoka Kiswahili hadi Ekegusii. (Shahada ya uzamili ya Kiswahili, haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Nairobi.

Mulalu, W. J; Kandargor, M. & Lonyangapuo, M. (2017). Sintaksia ya kirai kijalizo na uchopoaji wa viambajengo katika Kiswahili. Nairobi Journal of Humanities and Social Sciences, 9(1), 1-29.

Mutai, W. G. (2019). Muundo na uamilifu wa chagizo katika virai na vishazi vya Kiswahili sanifu. (Tasinifu ya shahada ya uzamili). Chuo Kikuu cha Nairobi.

Mkilima, F. (2020). Uainishaji wa Kategoria ya Kihusishi katika lugha ya Kiswahili. Jarida la CHALUFAKITA, 2, 1-14.

Mtego, D. R. (2022). Ruwaza za ujalizaji wa vitenzi vya Kiswahili sanifu. Kioo cha Lugha. 20(2), 285-304.

Nainggolan, I. A; Trilaksono, V. J; Silaban, N. M. & Munthe, R. V. M. (2024). Understanding subject complements in English Grammer. Halaman, 8(2),1-2.

Opoku, K. (2024). The term “complement” in systemic functional grammer: A review of its theoretical problems and implications. Open Journal of Modern Linguistics, 14,8-38.

Philipo, Z. T. & Kuyenga, F. E. (2017). Sintaksia ya Kiswahili: Nadharia za kisintaksia za uchanganuzi wa Kiswahili. Karljamer Publishers Limited.

Plag, I. (2003). Word formation in English. Cambridge University Press.

Quirk, R. & Greenbaum, S. (1986). A university grammar of English. Longman Group Limited.

Radford, A. (2004). English syntax: an introduction. Cambridge University Press.

Schafer, M. (2017). The semantic transparency of English compound nouns. Language Science Press.

Stephano, R. (2023). Utabirifu wa makosa ya utenganishaji na uunganishaji wa maneno katika Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dodoma.

Thompson, G. (2014). Introducing functional grammer (3rd ed.). Routledge.

TUKI (2004). Kamusi ya Kiswahili sanifu. TUKI.

Wesana-Chomi, E. (2017). Kitangulizi cha muundo viambajengo wa sentensi za Kiswahili. TUKI.

Young, P. V. (1984). Scientific social survey and research. Prentice Hall Inc.

Tarehe ya Uchapishaji
14 Julai, 2025
Jinsi ya Kunukuu
Mwampamba, A., & Labiswai, L. (2025). Uangavu wa Maana kama Nyenzo ya Ujalizaji katika Lugha ya Kiswahili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 8(2), 97-106. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3318