Usawiri wa Vyombo vya Dola katika Tamthilia ya Kilio cha Haki (1981) Kifo Kisimani (2001) na Upepo wa Mvua (2013)

  • Mutegi Dolly Kendi Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Murithi Joseph Jesse Chuo Kikuu cha Kenyatta
##plugins.pubIds.doi.readerDisplayName##: https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3334
##share.article##:

Résumé

Vyombo vya Dola ni taasisi za serikali zilizopewa mamlaka kikatiba kutekeleza sheria na kuendesha maswala ya nchi. Usalama na ulinzi wa nchi uhakikiswa kupitia kwa taasisi hizi. Umuhimu wake katika maisha ya binadamu ni wa juu zaidi. Fasihi ni kioo cha jamii na huyasawiri mambo yaliyopo na yanayotendeka katika jamii katika ukamilifu wake. Katika makala hii tulichambua namna waandishi wa tamthilia teule wanavyozisawiri taasisi hizi katika tamthilia zao. Tulitumia mbinu ya kusoma kwa kina maktabani kukusanya data ya utafiti. Nadharia ya mabadiliko iliyoasisiwa na Kurt Lewin ndiyo iliyotuongoza katika utafiti wetu iliyotusaidia kubaini utenda kazi wa Vyombo vya Dola na mabadiliko yaliyotokea katika utendakazi wa taasisi hizi katika mpito wa wakati. Tulibainisha kuwa taasisi hizi ni dhulumu na hutumiwa kutimiza matakwa ya viongozi au serikali iliyo hatamuni badala ya kushughulia wanajamii. Taasisi hizi huishia kukiuka sheria kwa kulinda na kutunza masilahi ya kisiasa na ya kiuchumi ya watawala badala ya kutetea haki za mtu binafsi. Mabadiliko yamepatikana kwa kiasi fulani hasa baada ya kuidhinishwa kwa katiba mpya ya mwaka 2010 iliyopendekeza mageuzi mbalimbali katika taasisi hizi. Baadhi ya taasisi hizi bado ziliendeleza dhuluma, japokuwa sasa kwa njia fiche si kwa njia ya uwazi. Japokuwa   mabadiliko hayajapatikana kwa ukamilifu, hatua kubwa zimepigwa na mchakato huu endelevu unazidi kutiliwa mkazo. Makala hii inapendekeza kuwepo na sheria na kanuni na njia mbadala za kuwajibisha Vyombo vya Dola ili taasisi hizi ziweze kutumikia jamii pana na kuwepo na imani na amani katika ya asasi za utawala na wanajamii. Uwajibikaji huu utasaidia kuondoa ukatili na dhuluma inayoendelezwa na taasisi hizi kwa wanajamii na kuhakikisha kuwa japokuwa vikosi hivi viko chini ya uongozi wa serikali, havitumiwi na serikali na watawala kudumisha nguvu zao za kiutawala.

##plugins.generic.usageStats.downloads##

##plugins.generic.usageStats.noStats##

Références

Amutabi, M. N. (2009). Beyond imperial presidency in Kenya: Interrogating the Kenyatta, Moi and Kibaki regimes and implications for democracy and development. Kenya Studies Review, 1(1), 55-84.

Hallinger, P., & Heck, R. H. (2007). Leadership for learning. Does collaborative leadership make a difference, 654-678.

Kothari, C. R. (2004). Research methodology: Methods and techniques. New Age International.

Kwaka, J., & Mutunga, T. M. (2011). Contemporary Kenya and its Leadership. Okombo, DN (2011). Challenging the Rulers: A Leadership Model for Good Governance, 1-12.

Mohajan, H. K. (2018). Qualitative research methodology in social sciences and related subjects. Journal of economic development, environment and people, 7(1), 23-48.

Mugenda, O. M. & Mugenda, A. G. (2003). Research Methods: Quantitative and Qualitative Approaches. Nairobi: ACTS Press.

Mukaria, A. R. (2018). Police Brutality in Kenya: Is it “utumishi kwa wote ama utumishi kwa wanasiasa” (service to all or to politicians)? (Master's thesis).

Muusya, J. K., King’ei, K., & Wafula, R. M. (2019). Uhusiano kati ya Asasi ya Familia na Uongozi wa Jamii katika Riwaya za Kiswahili Dunia Yao (Mohamed 2006) na Kidagaa Kimemwozea (Walibora 2012). Eastern Africa Journal of Contemporary Research, 1(1), 34-43.

Mwaniki, M. J., Timammy, R., & Ndung'u, M. N. (2021). Athari za Masuala ya Kijamii kwenye Mfumo wa Ikolojia Jamii: Uchanganuzi wa Diwani za Bara Jingine na Rangi ya Anga. Mulika Journal.

Wamitila, K. W. (2003). Kamusi ya fasihi: istilahi na nadharia.

Publiée
17 juillet, 2025