Maudhui ya Ukungwi katika Nyimbo Teule za Taarab

  • Fadhili Hamisi Wendo Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Kaui Titus, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Kungwi, Taarab, Unyago, Unyumba, Simiotiki, Nyimbo, Itikadi na Mwanamke
Sambaza Makala:

Ikisiri

Nyimbo za taarab zimetafitiwa na wataalam mbalimbali kwa mitazamo tofautitofauti. Kutokana na uchunguzi wa kina wa mtafiti, inabainika kuwa tafiti za awali kuhusu nyimbo za taarab, zimeegemezwa kwenye uchunguzi wa mafumbo katika taarab, masuala ya itikadi, nafasi ya mwanamke katika nyimbo za taarab usimulizi pamoja na uchanganuzi wa taswira katika nyimbo za taarab. Swala la jumbe za nyimbo za taarab kufungamana na mambo ya kijamii yakiwemo utamaduni limetajwa tu kijuujuu katika tafiti zao. Kutokana na upekuzi wa kina wa  mtafiti, hakuna utafiti ambao umefanywa kuhusu dhima ya kungwi inavyotekelezwa na baadhi ya nyimbo za taarab. Utafiti huu ulihusu ubainishaji wa maudhui ya ukungwi katika nyimbo teule za taarab. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Simiotiki. Nadharia hii  iliasisiwa na Ferdinand Dessaussure (1983)  na Charles Pierce (1998) na inahusu uhusiano uliopo kati ya kitaja na kitajwa na matumizi ya ishara, picha na msimbo. Nguzo hii ilisaidia katika kufafanua mbinu za uwasilishaji wa ujumbe katika nyimbo teule za taarab. Data ya kimsingi iliyoichanganuliwa ilikuwa ya maktabani ambapo mtafiti alipakua nyimbo teule kutoka kwenye mtandao wa You Tube na kuzichanganua kwa kina. Matokeo yalionyesha kuwa kungwi ana jukumu la kuwafundisha wanawari kuhusu masuala ya unyumba yakiwemo usafi wa mwili na nyumba, namna ya kumhudumia mume, namna ya kusema na marafiki na jamaa za mume, matumizi ya vifaa vya kiasili kama vile mbuzi, kinu, mchi ufagio miongoni mwa mengine. Aidha, maudhui haya ya ukungwi yanafundishwa na waimbaji wa nyimbo teule za taarab

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abdalla, A.R. (2018). Kuchunguza dhamira na fani katika nyimbo teule za taarab Asilia: Mifano ya nyimbo za Shakila Saidi Khamis. Tasnifu ya uzamili. Chuo kikuu cha Huria, Haijachapishwa.

Askew, K. M. (2002). Performing the Nation: Swahili Music and Cultural Politics in Tanzania. Chicago and London: University of Chicago Press.

Barthes, R. (1994). The Simiotic Challenge. University of California Press.

Fair, L. (1996). Identity, difference, and dance: Female initiation in Zanzibar, 1890 to 1930. Frontiers: A Journal of Women Studies, 17(3), 146-172.

Fair, L. (2001). Pastimes and politics: Culture, community, and identity in post-abolition urban Zanzibar, 1890–1945. Ohio University Press.

Gagliardi, P.L., Rocco, C. J., & Caravaggi, A. (2018). Navigation and Homing in Pigeons: A review of evidence and theories. Journal of Avian Biology, 49(8), 911-924.

Gikandi, S. (2000). Literary Theory and Criticism: The Use of Satire and Parody in Kiswahili Literature. Nairobi: East African Educational Publishers.

Khamis, A. (2015). Usiri katika Mafunzo ya Unyago: Mjadala wa Kijinsia na Utamaduni katika Jamii za Waswahili. Journal of Swahili Studies, 22(1), 45-60.

Khatib, M.S (1992). Taarab Zanzibar, Dar es salaam.Tanzania Publishing House.

Kirimi, M. J. (2015). The transformation of Swahili Unyago and female genital mutilation into an alternative rite of passage: a post structuralist approach.

Mehrabian, A. (1971). Silent messages: Implicit Communication of Emotions and Attitudes. Wadsworth Publishing.

Mwangangi, R. (2018). Mafunzo ya biashara za mtumba na athari zake kwa uchumi wa taifa. Chuo Kikuu cha Nairobi.

Makila, F. E. (20111.Uchunguzi wa nyimbo za Kiswahili: Mtazamo wa kifasihi. Nairobi: Tunaweza Publications

Ngwabi, R. (2020). The Role of Wisdom Figures in Community Development: A Study of Kungwi in African Societies. Journal of African Studies, 45(3), 25-39.

Okpewho, (1992). African Bloomington and Indianapo. Indiana University Press.

Pierce, C.S. (1998). The Essential Peirce: Selected Philosophical Writings (Vol. 1). Indiana University Press.

Rajab, F.H. (2016). Chanjo ya mapenzi katika nyimbo Asilia za Seif Salim. Tasnifu ya uzamili Chuo kikuu cha Tanzania, Haijachapishwa.

Saumu, A. (2011). Jinsi ya mwanamke kujipamba mwili. (Tasnifu ya shahada ya kwanza ya uzamili, Chuo Kikuu Kenyatta, Kenya.

Ferdinand, D. (1993). Course in General Linguistics (Trans. Roy Harris) London. Duckworth.

Strobel, M. A. (1984). In Women leaders in Africa history (Ed.), Heinemann.

Tenge, S. (2019). Usimamizi wa Biashara na Athari za Mbinu za Haraka katika Utendaji wa Muda Mrefu. Chuo Kikuu cha Nairobi.

Trimigham, J. S. (1980). The influence of Islam upon Africa. Longman Group Ltd, London.

Wamitila, K. W. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake. Phoenix Publishers.

Wright, W. (1975). Six guns and society: A structural study of the Western.

Yego, R.E. (2013). Nafasi ya mwanamke: Jinsi inavyotoweka kaika nyimbo za taarab Asilia za Zanzibar. Tasnifu ya uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi. Haijachapishwa.

Tarehe ya Uchapishaji
18 Julai, 2025
Jinsi ya Kunukuu
Wendo, F., & Titus, K. (2025). Maudhui ya Ukungwi katika Nyimbo Teule za Taarab. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 8(2), 119-132. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3347