Mtagusano wa Kimofofonolojia katika Kiolezofaridi cha Lugha ya Kiswahili: Mapengo ya Kiolezofaridi
Ikisiri
Makala hii inalenga kubainisha mapengo kwenye violezofaridi vya kimofofonolojia katika lugha ya Kiswahili. Kiolezofaridi ni mfumo wa mpangilio wa vipengee vya kiisimu ambao unaonyesha uhusiano wima baina ya kipashio kimoja na vipashio vingine katika muktadha maalum, yaani ni mfumo wa miundo ya kisarufi. Pengo la kimofofonolojia hutokea pale ambapo kipashio fulani cha lugha kinakubalika licha ya kuwa kimekiuka sheria za uundaji na mnyambuliko wa maneno. Pia hutokea pale ambapo hata baada ya kuzingatia sheria hizi tunapata kipashio ambacho hakikubaliki katika lugha. Katika utafiti huu, kuna maumbo yanayotii kanuni za kisarufi lakini hayakubaliki kiisimu ilhali kuna yale ambayo yamekaidi kaida za kisarufi lakini yanakubalika. Katika mofolojia, kanuni za kimofolojia zinapokiukwa katika uambishaji, tunatarajia kuwa maumbo yatakayozalishwa yatakuwa na makosa ya kisarufi na hivyo kutotumika. Kwa upande mwingine, maumbo ya lugha yanapokubalika licha ya kutozingatia kanuni za kimofolojia ni ishara kuwa kuna pengo la kiolezofaridi katika kiwango cha kimofolojia. Mofolojia hutagusana sana na michakato ya kifonolojia; hivyo basi katika makala hii tutashuhudia jinsi fonolojia inavyoathiri kiolezofaridi cha kimofolojia. Nadharia ya Kiolezofaridi Bora (Optimal Paradigms) iliyoasisiwa na McCarthy (2005) ndiyo iliyotumika. Misingi ya nadharia hii ni; kwanza, mshindani huzingatia vielelezo vya unyambuaji pale ambapo kiolezo cha unyambuaji huwa na maneno yaliyojikita kwenye msamiati mmoja. Pili, mashartizuizi ya uadilifu na uziada hutathmini washindani. Ukiukaji wa mashartizuizi wa kila kipashio hujumuishwa. Tatu, maumbotokeo hufanana na vielelezo vya vipashio vingine na hatimaye kuna makundi ya maumbotokeo ya mashartizuizi ya uadilifu yanayofanana. Data ya utafiti huu ilikusanywa maktabani na mtandaoni. Watafiti walisoma kwa kina vitabu vya lugha ya Kiswahili ambavyo vimechapishwa, tasnifu za lugha na pia, makala zilizochapishwa mtandaoni ili kupata data iliyohitajika. Asili ya data ni matini teule za isimu na data yenyewe ni violezofaridi vyenye mapengo. Usampulishaji dhamirifu ulitumika kuteua kazi za isimu. Data iliteuliwa kimakusudi na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo na majedwali. Matokeo ya utafiti huu yaliweka wazi kuwa mapengo katika lugha ya Kiswahili husababishwa na hali mbalimbali. Utafiti huu umebainisha kuwa katika lugha Kiswahili, mapengo ya violezofaridi yapo kwenye matawi ya fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki.
Upakuaji
Marejeleo
Baronian, L. & Kulinch, E. (2012). Paradigm Gaps in Whole Word Morphology. Akademia Verlang.
Bonet, E. & Lloret, M. (2002) pp19-39. OCP Effects in Catalan Cliticization. Barcelona: Catalan Journal of Linguistics, Vol 1. From http://seneca.uab.es/ggt.Reports/GGT-01-1-14.12/12/2022
Fromkin, V. & Rodman, R. & Hyams, N. (2019). An Introduction to Language: Tenth Edition. California: Harcourt Brace College Publishers.
Hartmam, R. & Stork, F. (1972). Dictionary of Language and Linguistics. Essex: Essex Publisher.
Kotowski, S. na Plag, I. (2023). The Semantics of Derivational Morphology. Berlin; Boston : De Gruyter.
Lindfors, A. (2003). The -ku- Marker in Swahili. Uppsala: Uppsala University.
Marten, L. (2002). 87-100. A Lexical Treatment for Stem Marker in Swahili. Afrikanistische Arbeitspapiere 72. Swahili Forum. IX
Matthew, P. (1991). Morphology. Cambridge: Cambridge University Press.
McCarthy, J. (2005). Optimal Paradigms. Boston: University of Massachusetts.
McCarthy, J. (1998). Morpheme Structure Constraints and Paradigm Occultation. Chicago, IL: Chicago Linguistic Society.
McCarthy, J. & Prince, A. (1993). Prosodic Morphology: Constraint Interaction and Satisfaction. Amherst, M.A: University of Massachusetts.
Prince, A. & Smolensky, P. (2002). Optimality Theory: Constraint Interaction in Generative Grammar. New Jersey: Rutgers University.
Sims, A. (2006). Minding the Gaps: Inflectional Defectiveness in a Paradigmatic Theory. Ohio State University.
Stump, G. & Finkel, A. (2013). Morphological Typology: From Word to Paradigm. Cambridge: Cambridge University Press.
Tesar, B. & Smolensky, P. (2000). Learnability in Optimality Theory. Cambridge: MIT Press.
Copyright (c) 2025 Naomi Ndumba Kimonye, Leonard Chacha Mwita, Peter Githinji

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.