https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/issue/feed East African Journal of Swahili Studies 2025-08-25T20:52:56+02:00 Prof. Jack Simons editor@eanso.org Open Journal Systems <p>The development of Swahili as a language is important in the development and preservation of indigenous culture, knowledge and religion in Swahili speaking regions in Africa. This peer-reviewed journal therefore exclusively published only Swahili articles. The articles publishable under this journal range from all genres of knowledge provided that they are written in Swahili language.&nbsp; Authors submitting to this journal can however decide to translate their articles into English and publish the translations in any other of our hosted journals.</p> https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3247 Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu 2025-07-02T15:51:34+02:00 Jackline Osagi Mwanzi jacklinemwanzi@yahoo.com <p>Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika ngazi ya kitaifa nchini Kenya ambapo mfumo wa elimu wa 8-4-4 unaondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na mtaala wa umilisi (CBC). Mabadiliko haya yamejikita katika elimu ya msingi, kuanzia kiwango cha chekechea, shule za upili hadi kwenye vyuo vinavyotoa elimu ya kiufundi kote nchini. Kwa sasa, mabadiliko katika mtaala wa kitaifa hayajaathiri vyuo vikuu kunakotolewa elimu ya juu. Hata hivyo, wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu huandaliwa kupitia kwa mafunzo ya shule za upili. Hivyo basi mabadiliko yoyote yanayotokea katika elimu ya msingi lazima yataathiri programu za mafunzo yanayotolewa katika vyuo vikuu. Makala haya yataangazia kipengele cha tathmini katika vyuo vikuu kwa kuzingatia mabadiliko katika mfumo wa elimu uliopo na vigezo vinavyoelekeza tathmini katika mfumo wa elimu wa umilisi. Mabadiliko katika tathmini katika mfumo wa elimu wa umilisi yanaashiria kuwepo haja ya kufanya mabadiliko sawia ya tathmini katika mafunzo ya elimu ya juu katika vyuo vikuu. Hali hii inatokea kuwa hivi kwa kuwa wanafunzi wanapojiunga na vyuo vikuu watakuwa wamezoeshwa tathmini ya shule za upili ambayo hufanyika katika kila hatua ya ujifunzaji mafunzo yanapoendelea tofauti na illivyokuwa awali ambapo tathmini ilifanyika mara moja mwishoni baada ya kipindi maalumu cha mafunzo (mwishoni mwa miaka minane katika shule za msingi na miaka minne katika shule za upili). Swali hapa ni je, tathmini ya awali iliyozoeleka na ambayo ilifanyika baada ya kipindi maalumu bado itafaa? Bado itafikia malengo yaliyopo ya elimu? Kufikia sasa, hakuna mwelekeo wowote ambao umetolewa kuhusiana na hili. Hali hii inapelekea kuwepo haja ya kubuni sera itakayotoa mwelekeo kuhusu vigezo vinavyofaa kuzingatiwa katika kubadili tathmini katika vyuo vikuu ili iendane na mabadiliko yanayoendelea kutokea katika mfumo wa elimu uliopo. Mabadiliko katika tathmini vyuoni yanaweza kufanyika kwa kulinganisha na kulinganua tathmini iliyokuwepo awali na iliyopo hivi sasa katika elimu ya msingi na vyuo vikuu. Makala haya yamechanganua changamoto zinazotokana na hiyo mifumo miwili ya tathmini na kuangazia namna ambavyo aina zote mbili za tathmini humwathiri mwanafunzi ambaye ndiye mwathiriwa mkuu. Makala haya yamelenga kuwezesha vyuo vikuu kutambua mielekeo na mitazamo ambayo wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga navyo huingia nayo vyuoni kutokana na namna wanavyotathminiwa wanapopokea elimu ya msingi. Makala haya yametokana na uchambuzi na mapitio ya maandishi yaliyopo tayari kuhusu mifumo hii miwili ya elimu pamoja na maoni ya wataalamu wa masuala ya mitaala. Maandishi haya yalipatikana maktabani na mitandaoni.</p> 2025-07-02T15:13:19+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3248 Vichocheo Vinavyowafanya Wahudumu wa Bodaboda na Abiria Kuzingatia au Kukiuka Upole Katika Mawasiliano 2025-07-02T15:51:34+02:00 Faith Mbithe Kathukya faithmbithe202@gmail.com John Khaisie Wanyama, PhD khaisie.john@embuni.ac.ke Timothy Kinoti M’ngaruthi, PhD mngaruthi.timothy@embuni.ac.ke <p>Upole ni muhimu katika kufanikisha mawasiliano. Husaidia katika kukabiliana na matendo ya kutishia uso. Utafiti huu ulilenga kuchunguza kuhusu sababu zinazowachochea wahudumu wa bodaboda na abiria kuzingatia au kukiuka matumizi ya mikakati ya upole katika mawasiliano yao. Nadharia ya upole ndiyo iliyotumika kuelekeza utafiti huu.&nbsp; Utafiti ulifanyika katika kaunti ndogo ya Mbooni iliyo katika kaunti ya Makueni, nchini Kenya.&nbsp; Walengwa walikuwa ni wahudumu wa bodaboda na abiria walioteuliwa kimakusudi hadi pale ambapo kiwango kifu kilifikiwa. Utafiti huu wa kithamano, ulitumia mbinu ya uchunzaji na mahojiano katika kukusanya data. Uchanganuzi wa kimaudhui ulitumika ili kuhakiki majibu ya mahojiano kwa kuelekezwa na mihimili ya nadharia. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa kuna sababu kadhaa zinazochochea hali ya kuzingatia au kukiuka matumizi ya mikakati ya upole katika mawasiliano. Sababu hizo ni kama vile: faida tarajiwa, tofauti za mahusiano, haja ya kutaka kuonyesha heshima kwa sababu ya tofauti za kimamlaka na hali ya kutaka kukabiliana na uzito wa tendo la kutishia uso. Faida au matokeo tarajiwa yalichochea uzingatiaji wa mikakati ya upole sana. Sababu hii ilijitokeza kwa wingi kwani mawasiliano yalitokea katika muktadha wa uchukuzi ambapo mantiki huzingatiwa sana ili kufikia malengo ya kibiashara. Hivyo, wahudumu wa bodaboda na abiria walizingatia zaidi mafanikio ya mawasiliano kuliko vipengele vya kijamii. Matokeo ya utafiti huu yanaiarifu nadharia kwani yanaonyesha kuwa mbali na vigezo vya kijamii vinavyosisitizwa na nadharia, faida tarajiwa huchochea matumizi ya mikakati ya upole katika muktadha wa uchukuzi. Utafiti huu una umuhimu kwa taaluma ya mawasiliano hasa kwa kurahisisha maingiliano baina ya watu katika jamii. Isitoshe utakuwa wenzo muhimu kwa watafiti wa baadaye watakaojihusisha na uga wa pragmatiki</p> 2025-07-02T15:19:46+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3256 Utafiti wa Lahaja Kupitia Macho ya Jamii: Matumizi ya Mtazamo Tambuzi wa Elimu Lahaja Katika Kaunti ya Lamu 2025-07-03T14:48:31+02:00 Judy Wangari Onyancha judynyamweya16@uonbi.ac.ke Rayya Timammy rayya@uonbi.ac.ke Mungai Mutonya mmutonya@wustl.edu <p>Utafiti huu unachunguza uainishaji wa mipaka ya lahaja za Kiswahili zinazozungumzwa katika Kaunti ya Lamu, Kenya, kwa kutumia nadharia ya Mtazamo Tambuzi wa Elimu Lahaja (Preston, 1989). Tofauti na tafiti za awali zilizozingatia vipengele vya kimuundo vya lugha, utafiti huu umejikita katika maoni, mitazamo, uelewa na hisia za wasemaji wazawa kama vigezo halali vya kutambua na kuainisha lahaja. Kwa kutumia mbinu ya uchoraji wa ramani za mikono, sauti zilizorekodiwa, na mijadala ya vikundi, washiriki waliainisha maeneo ya lahaja kwa msingi wa tajriba zao binafsi. Data hiyo ilichakatwa kwa kutumia teknolojia ya GIS (QGIS na ArcGIS) kwa njia ya <em>Kernel Density Estimation</em> (KDE). Matokeo yameonyesha kuwepo kwa makundi makuu manne ya lahaja: Kiamu, Kipate, Kisiu na Kitikuu, huku Kishela na Kimatondoni zikiwa kwenye hatari ya kufifia kutokana na ushawishi wa Kiamu. Aidha, vipengele vya kifonolojia, kimofolojia na kisintaksia vilijitokeza kuwa msingi wa utambuzi wa tofauti hizo. Imebainika kuwa asili ya mzungumzaji, uzoefu wa lugha, na uhusiano wa kijamii ni vigezo muhimu vinavyoathiri namna wanavyotambua na kuchora mipaka ya lahaja. Utafiti huu unatoa mchango mpya kwa taaluma ya isimu-jamii na lahaja kwa kusisitiza umuhimu wa data tambuzi kutoka kwa jamii, na hivyo kupanua upeo wa utafiti wa lugha za Kiafrika kutoka katika mtazamo wa jamii kuelekea usomi wa kitaaluma</p> 2025-07-03T13:59:28+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3257 Unyanyasikaji wa Wanaume katika Diwani za Tumbo Lisiloshiba na Maskini Milionea na Hadithi Nyingine 2025-07-03T14:48:31+02:00 Elizabeth Wanjiru Waithaka ewwanjiru84@gmail.com John Khaisie Wanyama, PhD khaisie.john@embuni.ac.ke Timothy Kinoti M’ngaruthi, PhD mngaruthi.timothy@embuni.ac.ke <p>Fasihi kama kioo cha jamii hutumia lugha kwa ufanifu mkubwa kutuchorea taswira kamili ya yale yanayotendeka katika jamii. Fasihi haizuki katika ombwe tupu. Hivyo basi utafiti huu ulichunguza unyanyasikaji wa wanaume katika jamii. Ulichunguza suala mtambuko ambalo linaathiri haki za wanaume kama inavyosawiriwa katika Diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine iliyohaririwa na Alifa Chokocho na Dumu Kayanda na Maskini Milionea na Hadithi Nyingine iliyohaririwa na Ken Walibora. Lengo kuu la makala hii ni kuchunguza namna wanaume hunyanyasika katika diwani teule. Ilikuafikia lengo hili, nadharia ya Mtagusano wa Vitambulisho ilitumiwa. Ni mojawapo ya nadharia za kijinsia. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktaba. Data ya utafiti ilikusanywa kwa kusoma hadithi teule kutoka diwani za Kiswahili zilizoteuliwa vitabu, majarida na makala mengine kutoka mitandaoni. Uteuzi wa sampuli ulikuwa wa kimaksudi. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kimaelezo kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi matini ikiongozwa na madhumuni ya utafiti. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Matokeo ya makala yalionyesha kuwa mwanamume hunyanyasika kwa namna nyingi kama vile: kula uroda nje ya ndoa, utengano wa kijamaa, kukataliwa uchumba, upyaro, kunyimwa chakula na kuchapwa. Vipengele vya utambulisho vinavyoshirikiana na kusababisha unyanyasikaji wa wanaume ni: uchumi, jinsia, tabaka, matarajio ya kijamii. Kipengele kinachosababisha unyanyasikaji wa wanaume zaidi ni kipengele cha uchumi. Uchunguzi huu utawafaa wasomi, wanajamii, na waandishi kwani watapata uelewa zaidi wa aina za unyanyasikaji unaotendewa wanaume na kutafuta mbinu za kuwaokoa kutoka kwa udhalimu huu. Vile vile utakuwa na mchango katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili.</p> 2025-07-03T14:03:43+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3277 Mbinu za Kifasihi katika Uundaji na Uhawilishaji wa Maarifa Kupitia Bembezi za Jamii ya Watumbatu 2025-07-07T15:38:22+02:00 Riziki Pembe Juma rizikijamal@yahoo.com <p>Makala hii inachunguza mbinu za kifasihi zinazotumika kuunda bembezi za jamii ya Watumbatu kwa lengo la kubaini mchango wake katika uhifadhi wa maarifa ya kijamii, utamaduni na maadili. Utafiti huu ulifanyika Zanzibar, ukilenga kuchambua vipengele vya kifasihi vilivyomo katika bembezi kwa kutumia Nadharia ya Fasihi Simulizi. Mbinu za ukusanyaji wa data zilihusisha mahojiano, usikilizaji wa nyimbo na uchambuzi wa matini za fasihi simulizi. Data iliyokusanywa ilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa maudhui (Krippendorff, 2004), ambapo matokeo yanaonesha kuwa bembezi za Watumbatu zinatumia mbinu mbalimbali za kifasihi kama semi, tamathali za semi, usimulizi, vipamba-sauti, majazi na usambamba. Semi zilizotumika ni pamoja na methali, nahau na misemo inayobeba maana za kihisia na mafunzo ya kijamii, jambo linalothibitisha umuhimu wa lugha katika kujenga utambulisho wa jamii (Wamitila, 2003). Tamathali za semi kama tashbiha, sitiari na takriri huimarisha maana na mvuto wa lugha ya bembezi, huku usimulizi wa nafsi ya kwanza, pili na tatu ukitumiwa ili kuwafanya watoto washiriki na kuelewa nyimbo hizi kwa undani. Vipamba-sauti kama takriri na urari wa vina husaidia kukumbuka na kuelewa nyimbo kwa urahisi, huku majazi na usambamba vikiongeza mshikamano wa maudhui. Uchunguzi huu unathibitisha kuwa bembezi si nyimbo za kuburudisha pekee, bali ni chombo muhimu cha uhifadhi wa maarifa, uhamasishaji wa lugha na uendelezaji wa utamaduni wa jamii ya Watumbatu. Tafiti zaidi zinahitajika kuchunguza bembezi katika jamii nyingine za Kiswahili ili kubaini athari zake kwa maendeleo ya lugha na elimu ya watoto.</p> 2025-07-07T15:36:56+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3281 Ujenzi wa Sifa za Mhusika wa Riwaya ya Kiswahili: Tathmini ya Mchango wa Mandhari katika Kiu na Kidagaa Kimemwozea 2025-07-07T19:18:41+02:00 Wyckliffe Collins Jaoko wycliffe.collins@yahoo.com Stanley Adika Kevogo surayangu@gmail.com <p>Mandhari hufasiliwa kuwa ni wakati na mahali patendekapo kadhia, visa au matukio katika utungo wa kifasihi unaohusika. Mandhari yanaweza kuwa halisi au ya kufikirika. Utafiti ulioichipuza makala hii uliazimia kuchunguza usawiri wa mandhari katika riwaya ya Mohamed S. Mohamed, Kiu pamoja na ile ya Ken Walibora, Kidagaa Kimwemwozea. Ingawa malengo muhsusi ya utafiti yalikuwa matatu, makala hii inazamia lengo moja tu - kutathmini mchango wa mandhari katika ujenzi wa sifa za wahusika katika riwaya ya Kiu na Kidagaa Kimemwozea. Tathmini yenyewe imekitwa kwenye mseto wa nadharia mbili - Uhalisia na Umuundo. Nadharia ya Uhalisia inachimuza uyakinifu wa mandhari ya kijamii ilhali nadharia ya Umuundo ikasisitiza dhima na uhusiano wa vipengele vya sanaa. Utafiti huu wenye mkabala wa kithamano ulifanywa maktabani kwa kuzingatia muundo wa kiuchanganuzi. Eneo la utafiti ni fasihi andishi, hususan utanzu wa riwaya ya Kiswahili. Idadi lengwa ya utafiti ni riwaya 10 za kiuhalisia zinazosawiri mandhari halisi. Sampuli ya riwaya mbili, Kiu na Kidagaa Kimemwozea, iliteuliwa kwa usampulishaji dhaminifu. Riwaya hizi ziliteuliwa kwa misingi ya wingi wa vifani vilivyochunguzwa, yaani usawiri wa mandhari. Pamoja na kuakisi malengo ya utafiti, utunzi wa riwaya teule unaambatana na mihimili ya mseto wa nadharia za utafiti. Data msingi ya utafiti ilikusanywa kwa usomaji wa kina wa matini za riwaya teule. Nazo data za upili zikakusanywa kwa usomaji wa kina wa vitabu, tasnifu na makala anuwai za kitaaluma. Data zilizokusanywa ziliainishwa kwa mujibu wa mihimili ya nadharia na malengo ya utafiti. Zilichanganuliwa kwa mujibu wa yaliyomo na matokeo kuwasilishwa kimaelezo. Matokeo ya utafiti yanadhihirisha kwamba mandhari yana mchango wa moja kwa moja katika ujenzi wa sifa za wahusika. Mandhari hayo ni kama vile: ya mahali(upembeni mwa Mto Kiberenge, chumba cha Mtemi Nasaba Bora, msituni, seli, chumba cha Mzee Mwinyi na mandhari ya mitaa kama wa vibyongoni, Selea, Ukele na mingineyo) na ya kiwakati (enzi za kikoloni,miaka mitano, Vitaa Vikuu vya Pili vya Dunia na kadhalika). Mandhari haya yalisukwa kwa ustadi ambao ulichangia ukuzaji wa sifa za wahusika kwa urahisi mno. Matokeo ya utafiti huu yana tija kwa wanariwaya na wahakiki wa kazi za kifasihi kwa jumla. Yatawasaidia kutunga visa vinavyosawiri na kuakisi mandhari kuntu. Isitoshe, wahakiki wa kazi za fasihi watawezeshwa kubaini na kutathmini mandhari anuwai pamoja na dhima zao katika kazi za kifasihi.</p> 2025-07-07T19:18:00+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3286 Mikakati ya Kimtindo katika Muziki wa Benga wa Jamii ya Wakamba: Mkabala wa Umtindo 2025-07-08T20:14:20+02:00 Carolyne Muthini Mutuku muthinimutuku707@gmail.com John Khaisie Wanyama, PhD khaisie.john@embuni.ac.ke Timothy Kinoti M’ngaruthi, PhD mngaruthi.timothy@embuni.ac.ke <p>Muziki wa benga ni utanzu maarufu nchini Kenya. Hujitambulisha kwa sifa ya mdundo na mapigo ya kasi pamoja na ustadi wa msanii wa kucheza gitaa na kuimba kwa mtindo maalum. Utafiti huu ulilenga kubainisha mikakati ya mtindo inayotumika katika muziki wa benga wa jamii ya Wakamba kujenga hisia na athari za kijamii. Uchunguzi huu uliongozwa na kielelezo cha Umtindo. Umtindo hufasiri na kuhakiki tungo kwa kuzingatia mtazamo wa kiisimu kama taaluma iliyo na uhusiano wa karibu na fasihi. Uchunguzi wa kimtindo huhusisha namna lugha inavyotumika katika matini ili kujenga maana na athari. Usampulishaji ulifanywa kimakusudi ambapo nyimbo tano za muziki wa benga wa jamii ya Wakamba ziliteuliwa. Ukusanyaji wa data ulihusisha upakuaji wa nyimbo za benga kutoka kwa mtandao wa kijamii wa <em>Youtube</em> na unakili wa mishororo yake. Mbinu ya uchanganuzi matini ilitumika kubainisha mikakati ya kimtindo na kuchanganuliwa kithamano kwa kuelekezwa na mihimili ya nadharia ya umtindo. Data zilikuwa ni maneno, dhana, kauli, virai na sentensi zinazotumiwa na waimbaji wa muziki wa benga wa jamii ya Wakamba zinazohusisha vipengele vya kimtindo. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kimaelezo. Ilibainika kuwa, waimbaji wa muziki wa benga wa jamii ya Wakamba hutumia mikakati ya kimtindo kama vile ugawaji wa beti, uradidi, urudiaji, tamathali za usemi na aina anui za sentensi kuwasilisha ujumbe. Utafiti huu ni muhimu katika kuufanya muziki wa benga wa jamii ya Wakamba kutambulika katika nyanja za utafiti wa kielimu wa fasihi na lugha kama kategoria ya nyimbo za kitamaduni. Utachangia taaluma ya isimu na mawasiliano kwa kuangazia baadhi ya teuzi za kiisimu zinazofanywa na wasanii</p> 2025-07-08T20:13:51+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3318 Uangavu wa Maana kama Nyenzo ya Ujalizaji katika Lugha ya Kiswahili 2025-07-17T07:09:24+02:00 Amulike Abraham Mwampamba amulikemwampamba@gmail.com Lohay Marko Labiswai markolabiswai964@gmail.com <p>Makala haya yanahusu uangavu wa maana kama nyenzo ya ujalizaji katika lugha ya Kiswahili. Lengo la makala haya ni kuonesha kuwa ujalizaji huwa wa lazima ili kukidhi uangavu wa maana na si kukidhi miundo pekee. Data za makala haya zimekusanywa kwa njia ya usomaji makini, kuchambuliwa kwa nadharia ya Uchambuzi wa Maudhui na kuwasilishwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Aidha, wataalamu wengi wanakieleza kijalizo kama kipashio mojawapo katika sentensi. Hata hivyo hawabainishi wazi ulazima wa kijalizo katika sentensi huukiliwa na nini. Baadhi wanataja tu kuwa kijalizo ni cha lazima katika muundo wa sentensi. Miongoni mwao ni Massamba (2004); Habwe na Karanja (2004); Koech (2013); Matei (2017); Philipo na Kuyenga (2017) na Mtego (2022). Makala yameonesha jinsi uangavu wa maana unavyokifanya kijalizo kuwa cha lazima katika sentensi za Kiswahili. Makala yamedhihirisha kuwa kijalizo huwa cha lazima si tu kukidhi miundo ya sahihi bali pia kukidhi uangavu wa maana katika sentensi za lugha. Matokeo ya makala haya yameonesha kuwa ujalizaji katika tungo si jambo la hiari bali ni hitaji la lazima. Ulazima wa ujalizaji katika tungo hutokana na ukweli kwamba ili tungo iwe na uangavu lazima pawepo ujalizaji. Kwa hiyo, mwandishi anapendekeza kwamba ujalizaji katika tungo usifanyike ili tu kukamilisha muundo wa tungo pekee bali ufanyike ili kuleta uangavu wa maana katika tungo. Kwa kuwa lengo la lugha ni kukidhi mwasiliano, tungo zenye uangavu utokanao na ujalizaji ndizo zenye uwezo wa kufikia hitajio hilo</p> 2025-07-14T19:09:46+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3334 Usawiri wa Vyombo vya Dola katika Tamthilia ya Kilio cha Haki (1981) Kifo Kisimani (2001) na Upepo wa Mvua (2013) 2025-07-17T08:13:51+02:00 Mutegi Dolly Kendi kendidolly94@gmail.com Murithi Joseph Jesse kendidolly94@gmail.com <p>Vyombo vya Dola ni taasisi za serikali zilizopewa mamlaka kikatiba kutekeleza sheria na kuendesha maswala ya nchi. Usalama na ulinzi wa nchi uhakikiswa kupitia kwa taasisi hizi. Umuhimu wake katika maisha ya binadamu ni wa juu zaidi. Fasihi ni kioo cha jamii na huyasawiri mambo yaliyopo na yanayotendeka katika jamii katika ukamilifu wake. Katika makala hii tulichambua namna waandishi wa tamthilia teule wanavyozisawiri taasisi hizi katika tamthilia zao. Tulitumia mbinu ya kusoma kwa kina maktabani kukusanya data ya utafiti. Nadharia ya mabadiliko iliyoasisiwa na Kurt Lewin ndiyo iliyotuongoza katika utafiti wetu iliyotusaidia kubaini utenda kazi wa Vyombo vya Dola na mabadiliko yaliyotokea katika utendakazi wa taasisi hizi katika mpito wa wakati. Tulibainisha kuwa taasisi hizi ni dhulumu na hutumiwa kutimiza matakwa ya viongozi au serikali iliyo hatamuni badala ya kushughulia wanajamii. Taasisi hizi huishia kukiuka sheria kwa kulinda na kutunza masilahi ya kisiasa na ya kiuchumi ya watawala badala ya kutetea haki za mtu binafsi. Mabadiliko yamepatikana kwa kiasi fulani hasa baada ya kuidhinishwa kwa katiba mpya ya mwaka 2010 iliyopendekeza mageuzi mbalimbali katika taasisi hizi. Baadhi ya taasisi hizi bado ziliendeleza dhuluma, japokuwa sasa kwa njia fiche si kwa njia ya uwazi. Japokuwa&nbsp;&nbsp; mabadiliko hayajapatikana kwa ukamilifu, hatua kubwa zimepigwa na mchakato huu endelevu unazidi kutiliwa mkazo. Makala hii inapendekeza kuwepo na sheria na kanuni na njia mbadala za kuwajibisha Vyombo vya Dola ili taasisi hizi ziweze kutumikia jamii pana na kuwepo na imani na amani katika ya asasi za utawala na wanajamii. Uwajibikaji huu utasaidia kuondoa ukatili na dhuluma inayoendelezwa na taasisi hizi kwa wanajamii na kuhakikisha kuwa japokuwa vikosi hivi viko chini ya uongozi wa serikali, havitumiwi na serikali na watawala kudumisha nguvu zao za kiutawala.</p> 2025-07-17T08:06:53+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3347 Maudhui ya Ukungwi katika Nyimbo Teule za Taarab 2025-07-18T13:49:16+02:00 Fadhili Hamisi Wendo fadhiliwendo5@gmail.com Kaui Titus, PhD kauititus@ku.ac.ke <p>Nyimbo za taarab zimetafitiwa na wataalam mbalimbali kwa mitazamo tofautitofauti. Kutokana na uchunguzi wa kina wa mtafiti, inabainika kuwa tafiti za awali kuhusu nyimbo za taarab, zimeegemezwa kwenye uchunguzi wa mafumbo katika taarab, masuala ya itikadi, nafasi ya mwanamke katika nyimbo za taarab usimulizi pamoja na uchanganuzi wa taswira katika nyimbo za taarab. Swala la jumbe za nyimbo za taarab kufungamana na mambo ya kijamii yakiwemo utamaduni limetajwa tu kijuujuu katika tafiti zao. Kutokana na upekuzi wa kina wa&nbsp; mtafiti, hakuna utafiti ambao umefanywa kuhusu dhima ya kungwi inavyotekelezwa na baadhi ya nyimbo za taarab. Utafiti huu ulihusu ubainishaji wa maudhui ya ukungwi katika nyimbo teule za taarab. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Simiotiki. Nadharia hii&nbsp; iliasisiwa na Ferdinand Dessaussure (1983)&nbsp; na Charles Pierce (1998) na inahusu uhusiano uliopo kati ya kitaja na kitajwa na matumizi ya ishara, picha na msimbo. Nguzo hii ilisaidia katika kufafanua mbinu za uwasilishaji wa ujumbe katika nyimbo teule za taarab. Data ya kimsingi iliyoichanganuliwa ilikuwa ya maktabani ambapo mtafiti alipakua nyimbo teule kutoka kwenye mtandao wa You Tube na kuzichanganua kwa kina. Matokeo yalionyesha kuwa kungwi ana jukumu la kuwafundisha wanawari kuhusu masuala ya unyumba yakiwemo usafi wa mwili na nyumba, namna ya kumhudumia mume, namna ya kusema na marafiki na jamaa za mume, matumizi ya vifaa vya kiasili kama vile mbuzi, kinu, mchi ufagio miongoni mwa mengine. Aidha, maudhui haya ya ukungwi yanafundishwa na waimbaji wa nyimbo teule za taarab</p> 2025-07-18T13:48:48+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3382 Athari ya Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia kwa Ujumbe wa Lugha Chanzi; Tafsiri Kutoka Kiswahili Kwenda Kiingereza 2025-07-24T19:33:27+02:00 Mutisya Cosmas Mbithi samwelngetich001@gmail.com Sarah Ndanu Ngesu, PhD cosmasmutisyam@gmail.com Esther N. Chomba, PhD cosmasmutisyam@gmail.com <p>Suala la athari katika uhawilishaji wa&nbsp; kwenye ujumbe wa lugha chanzi katika tafsiri si geni. Tafiti nyingi zimelishughulikia suala hili lakini tafiti hizo zimeegemea sana katika athari ya uhawilishaji wa ujumbe kutoka lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili. Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza athari ya uhawilishaji wa&nbsp; kwa ujumbe wa lugha chanzi katika tafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. &nbsp;Data za utafiti zilipatikana kwa kusoma, kuchanganua na kuhakiki tafsiri ya vitabu teule vya fasihi: <em>Siku Njema</em> ya Walibora (1996) na tafsiri yake <em>A Good Day</em> iliyotafsiriwa na Kweyu na Kawegere (2019), <em>Kaburi bila Msalaba</em> iliyoandikwa na Kareithi (1969) na tafsiri yake ya Kiingereza <em>Unmarked Grave</em> iliyotafsiriwa na Githiora (2019). Vilevile, mtafiti aliangazia tamthilia mbili; Tamthilia ya <em>Natala</em> iliyoandikwa na Mberia (1997) na tafsiri yake ya Kiingereza <em>Natala</em> iliyotafsiriwa na Kasu na Marami (2011). Tamthilia ya <em>Kinjekitile</em> iliyoandikwa na Hussein (1969) na tafsiri yake <em>Kinjekitile</em> iliyotafsiriwa na Hussein mwenyewe (1970) ilichunguzwa. Mtafiti aliteua vitabu hivi kwa kuwa vilionesha utajiri wa data inayohusu uhawilishaji wa jinsia. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya <em>Skopos</em> na Nadharia ya Usawa wa Kidhima. Nadharia ya <em>Skopos</em> iliyoasisiwa na Hanns Vermeer (1989) ambayo husisitiza kuwa, kimsingi kutafsiri kunafaa kushughulikia jukumu la matini chanzi na matini lengwa yaani tafsiri ni kitendo chenye malengo. Nadharia ya Usawa wa Kidhima iliasisiwa na Nida (1964) na inatilia mkazo usawa wa kimaana na athari sawa kwa hadhira katika mchakato wa tafsiri. Natharia hizi zilisaidia kuchuguza athari ya uhawilishaji wa kwa ujumbe asilia katika vitabu teule. Data ya utafiti huu ilipatikana kwa kusoma na kuainisha katika vitabu teule vilivyotafsiriwa kutoka kiswahili kwenda kiingereza. Baada ya kubainisha uhawilishaji wa data hiyo ilichanganuliwa kitaamuli na kitakwimu na matokeo kuwasilishwa kupita maandishi ya kinadhari majedwali na michoro ya miche duara kutathimini athari ya uhawilishaji huo kwa ujumbe wa lugha chanzi. Matokeo ya&nbsp; utafiti huu yanaonesha kuwa wafasiri wa vitabu teule wamehawilisha&nbsp; na uhawilishaji huo ukawa na athari kwa ujumbe asilia. Uhawilishaji wa unachangamoto nyingi kwa hivyo wafasiri wanapaswa kumakinika kwani, uhawilishaji wa huwa na athari hasi na chanya kwa hadhira lengwa. Utafiti huu unapendekeza utafiti zaidi kufanywa katika uhawilishaji wa viwakilishi vya nyakati katika tafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza kwani kama uhawilishaji wa , uhawilishaji wa viwakilishi vya wakati vilevile, vinaweza kuwa na athari kwa ujumbe asilia.</p> 2025-07-24T00:00:00+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3427 Tathmini Ya Sura Za Ufisadi Katika Riwaya Za Tom Olali Mafamba (2012) Na Watu Wa Gehenna (2012) 2025-08-04T22:34:29+02:00 Pauline Musyoki paulina.musyoki1@gmail.com Jessee Murithi, PhD paulina.musyoki1@gmail.com <p>Utafiti huu unaeleza sura tofauti za ufisadi. Mtafiti amefanya hivi kwa kushughulikia riwaya ya Mafamba (Olali, 2012) na Watu Wa Gehenna (Olali, 2012). Ufisadi ni suala tata ulimwenguni na hata nchini Kenya. Dhana hii ni pana ila maelezo yake katika fasihi ni finyu kwa kuwa, msisitizo umekuwa kwenye usimamizi wa fedha za umma. Kulingana na Tume ya EACC (2016) kipengele cha IV, ufisadi&nbsp; unahusu unyanyasaji katika ofisi za umma, upendeleo, hongo, ulaghai, ukosefu wa uaminifu katika ofisi za umma, kutolipa ushuru au ada yoyote ile na kutofuata sheria zilizohidhinishwa kuteua viongozi katika ofisi za umma. Mtafiti ameangazia masuala hayo kwa kutathmini riwaya teule kwa lengo la kubainisha namna masuala hayo yalivyosawiriwa na kuleta uwezekano wa sura tofauti za ufisadi. Wahakiki kama vile; Muthumbi (2005) anaeleza ufisadi kama wizi wa pesa, Ochenga (2008) anaelezea ufisadi kama matumizi mabaya ya pesa za umma, Mayiek (2015) Ufisadi ni wizi wa mali ya umma, Sereti (2016) Ufisadi ni hali ya kujilimbikizia raslimali za taifa, Mwaniki (2018) Ufisadi ni unyakuzi wa mali ya umma.wahakiki hawa na wengineo wameeleza ufisadi kama matumizi mabaya ya fedha za umma&nbsp; na ndio sababu utafiti huu umeangazia sura tofauti za ufisadi. Riwaya zimeteuliwa kimakusudi na zimeangazia sura tofauti za ufisadi hivyo zilitupa data mwafaka. Nadharia ya&nbsp; Udenguzi ilitumika. Nadharia ya Udenguzi ilihusishwa na Jacques Derrida (1962).Waitifaki wake ni pamoja na Foocult, Roland Barthes, Jean Baudrillar, Paul Deman, J. Hills Miller, Jacques Lacan Barbara Johnstone na wengineo. Kupitia mihimili ya nadharia hii mtafiti alieleza fasiri mbalimbali za ufisadi. Utafiti huu ulifanywa maktabani kwa kusoma vitabu&nbsp; teule,&nbsp; tasnifu, majarida na makala ya mitandaoni yanayohusiana na mada. Data ya kimsingi ilitolewa kwenye riwaya teule. Data hiyo ilichanganuliwa kwa kuzingatia malengo na nadharia inayoongoza utafiti. Matokeo yamewasilishwa kwa kutumia njia ya maelezo. Utafiti huu utakuwa muhimu kwa wasomi na jamii kwa jumla hasa kwa kuagazia suala tata la ufisadi.</p> 2025-08-04T22:33:43+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3469 Mikakati ya Ushawishi katika Manifesto ya Kenya Kwanza katika Uchaguzi Mkuu wa 2022 Nchini Kenya 2025-08-11T22:06:34+02:00 Nancy Chepkemoi Kones konesnancy2013@gmail.com Raphael Mwaura Gacheiya konesnancy2013@gmail.com <p>Utafiti huu ulishughulikia mikakati ya ushawishi katika manifesto ya Muungano wa Kenya Kwanza katika uchaguzi mkuu wa 2022 nchini Kenya. Ulichunguza iwapo mikakati hiyo ilichangia katika kujenga mvuto wa kisiasa na uungwaji mkono katika uchaguzi mkuu wa Kenya. Lengo mahususi la utafiti huu lilikuwa kuchunguza jinsi mikakati ya ushawishi ilisawirika katika manifesto. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi Hakiki wa Usemi kuchanganua namna lugha inavyotumika kisiasa. Utafiti ulikuwa wa kithamano na ulitekelezwa kwa kutumia mbinu ya kifasili. Sampuli teule ya kimakusudi ilihusisha manifesto ya Kenya Kwanza. Deta ilikusanywa kutoka kwenye tovuti ya Muungano wa Kenya Kwanza. Ilichanganuliwa kwa kuangalia maudhui ya lugha ya ushawishi. Matokeo yalionesha kuwa lugha katika manifesto ililenga kuibua matumaini na ahadi ya maisha bora kwa wananchi. Makala hii inachangia maarifa katika taaluma ya Isimu, hasa katika muktadha wa kisiasa. Pia, inawapa wagombezi wa siasa mwongozo wa kuunda manifesto zenye mvuto, na inasaidia mashirika ya utafiti wa kisiasa kubuni sera na miongozo bora ya uchaguzi</p> 2025-08-11T19:48:50+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3485 - 2025-08-13T20:23:40+02:00 Mukonambi Kekonen Stanley stanleymukonambi@gmail.com Titus Kaui, PhD kauititus@ku.ac.ke <p>Makala hii inachunguza ubainishaji wa wakaa katika hotuba teule za wanasiasa wa Kenya. Baadhi ya wanasiasa hutoa hotuba zinazovuta makini ya wasikilizaji na wafuasi wao kwa mitindo tofauti. Mojawapo wa mbinu hii ya kimtindo ni usimulizi. Wakaa ni mojawapo wa kipengele cha kimtindo katika usimulizi. Tafiti kadha zimefanywa kubainisha wakaa na matumizi yake katika tanzu za fasihi andishi na fasihi simulizi (taz. Kwaka; 2015; Khamis; 2015; Muiya; 2018; Kinga; 2020; Asige, 2021). Licha ya hayo, tafiti hizi za awali hazikushughulikia wakaa kwa kuhusisha moja kwa moja si hotuba tu bali hotuba za kisiasa. Ni katika msingi huu ndipo makala hii imechunguza jinsi wakaa inavyojitokeza katika hotuba teule za wanasiasa wa Kenya. Makala hii imeelekezwa na nadharia ya Naratolojia iliyoasisiwa na mwanafalsafa Plato katika chapisho lake <em>The Republic</em> na baadaye ikaendelezwa na mwanafunzi wake Aristotle (1920) aliyewasilisha mawazo yake katika chapisho la <em>The Poetics</em> na wananaratolojia wa hivi majuzi Gennette (1980), Prince (1982) na Rimmon-Kenan (2002). Uchunguzi huu ulizingatia mawazo yake Rimmon-Kenan. Naratolojia ni stadi ya aina ya utendaji kazi wa usimulizi. Huangalia undani wa vifaa vinavyoongoza maelezo ya simulizi na ufahamu wa utendaji kazi wake. Data iliyotumika katika makala hii imetokana na kusoma machapisho maktabani kama vile tasnifu, majarida na vitabu. Halikadhalika, utazamaji, usikilizaji na uchambuzi wa hotuba teule za wanasiasa Mhes. Kenyatta, Odinga na Ruto katika mtandao wa <em>YouTube</em> ulihusishwa. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwepo kwa vipengele vya wakaa vya mpangilio, muda na idadi au umara katika hotuba za wanasiasa. Isitoshe, imebainika kuwa kipengele hiki cha usimulizi kimetumiwa kuendeleza maudhui, fani za lugha na kuchimuza wahusika</p> 2025-08-13T20:22:23+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3510 Mtindo na Matumizi ya Lugha Katika Muziki wa Taarab : Mifano Kutoka Taarab za Kiswahili 2025-08-19T08:49:29+02:00 Felix Kwame Sosoo fksosoo@ug.edu.gh <p>Makala hii inajadili juu ya mtindo na matumizi ya lugha katika Muziki wa Taarab kwa kutumia mifano kutoka Taarab za Kiswahili. Kwa kutumia nadharia ya umuundo makala hii inaibua vipengele vya lugha vinavyotumika katika Taarabu, kuelezea dhima ya uteuzi wa vipengele vya lugha na kujadili dhamira zinazoibuka kutokana na matumizi ya vipengele vya lugha katika Taarab. Katika kufikia lengo hilo makala hii inajibu maswali yafuatayo; Je, ni vipengele vipi vya lugha vinavyojichomoza zaidi katika Taarab? Je ni kwa nini wasanii huamua kuteua kutumia vipengele hivyo vya lugha? Na, ni dhamira zipi zinazoibuka kutokana na matumizi ya vipengele hivyo vya lugha?</p> 2025-08-19T08:48:29+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3527 Athari za Ubadilishaji Msimbo Kanisani kwa Wasikilizaji: Mifano Kutoka katika Mahubiri ya Mchungaji Wilbroad Mastai 2025-08-21T14:46:13+02:00 Amulike Abraham Mwampamba amulikemwampamba@gmail.com <p>Utafiti huu ulihusu athari za ubadilishaji msimbo kanisani kwa kuchunguza mahubiri ya Mchungaji Wilbroad Mastai. Lengo la utafiti lilikuwa kubainisha athari za ubadilishaji msimbo kwa wasikilizaji wa mahubiri ya Mchungaji Wilbroad Mastai. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa njia ya hojaji katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, kata ya Kimara, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam. Kadhalika utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Maki ya Carol Myers-Scotton (1993). Utafiti ulitumia usampulishaji nasibu tabakishi kuwapata watoa taarifa hamsini (50). Matokeo ya utafiti yalionesha kuwa wasikilizaji wanapata athari chanya (41.2%) na hasi (58.8%) kutokana na ubadilishaji msimbo katika mahubiri ya Mchungaji Wilbroad Mastai. Kwa hiyo, kutokana na matokeo ya utafiti huu ni wazi kwamba ubadilishaji msimbo katika mahubiri ni jambo lisilokubalika kwa wengi. Hii ni kutokana na athari hasi kuwa katika kiwango cha juu ukilinganisha na athari chanya. Aidha, utafiti huu ulipendekeza kwamba tafiti zingine zifanyike kuhusu sababu za ubadilishaji msimbo katika mahubiri ya Mchungaji Wilbroad Mastai pamoja na kuchunguza athari za ubadilishaji msimbo katika dini zingine</p> 2025-08-21T14:02:24+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3531 Mtazamo Linganishi wa Itikadi katika Utenzi wa Mwanakupona na Mashairi ya Muyaka 2025-08-21T14:46:13+02:00 Doreen Nkatha nkathadoreen13@gmail.com Jessee Murithi, PhD murithijj2015@gmail.com <p>Makala hii imechunguza itikadi katika <em>Utenzi wa Mwanakupona</em> na mashairi ya Muyaka. Itikadi ni mawazo ambayo hujumuisha malengo, matamanio na matarajio, na matendo ya mtu. Dhana ya itikadi pia imefasiriwa kama matamanio, fikra, malengo na maelezo ya mtunzi kuhusu masuala ya kijamii ya kisiasa, kidini, na kiuchumi kwa ujumla wake.&nbsp; Hivyo, itikadi kama imani ambazo huelekeza matendo ya binadamu yeyote ulimwenguni zimewaathiri watunzi wa kazi hizi mbili kwa namna wanavyosawiri mitazamo yao kuhusu wanavyowasilisha. Huelekeza matendo yale mtunzi atakayowasilisha na namna atakavyowasilisha kazi yake. <em>Utenzi wa Mwanakupona </em>na mashairi ya Muyaka ni kazi zilizoandikwa katika kipindi kimoja lakini utofauti unajitokeza wa kimtindo. Kwa hivyo, ni muhimu kuchunguza na kuzilinganisha itikadi zilizowaongoza watunzi hawa. Nadharia ya itikadi; mikabala ya Karl Marx (1977), Louis Althusser (1981) na Antonio Gramsci (1985), ilitumika. Mkabala wa Karl Marx ulitumiwa sababu dhana ya "ung’amuzi potoshi," mkabala wa Althusser ulitumiwa kwani unaorodhesha vyombo vya kiitikadi na mkabala wa Gramsci ulitumiwa sababu ya dhana ya ukubalifu na ukawaida.&nbsp; Data ya makala hii ilikusanywa maktabani. Vitabu teule, majarida na makala kuhusu mada husika mtandaoni yalisomwa kwa kina na kuchambuliwa. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika katika uteuzi wa sampuli. Kutokana na data ya utafiti huu, imebainika kuwa itikadi zinazowaongoza Muyaka na <em>Mwanakupona</em> ni tofauti kwani wanasawiri kazi yao kwa namna tofauti ingawa walikuwa watunzi wa kipindi cha kirasimi. Muyaka ilibainika kuwa aliongozwa na itikadi ya mapinduzi ya nguvu, uhuru wa kiakili na ukandamizaji. <em>Mwanakupona</em> kwa upande mwingine imebainika ameongozwa na itikadi ya utiifu, ukubalifu na ukawaida na hata ubabedume. Makala hii inapendekeza kuwa tafiti zingine zaidi kuhusu itikadi zinaweza kufanywa kuhusu tenzi za mwanzoni na kuzilinganisha, mikabala mingine za itikadi pia inaweza kutumika na pia utafiti zaidi unaweza kufanywa kuhusu utenzi wa <em>Mwanakupona</em> kuhusu wanatapo wa tatu.</p> 2025-08-21T14:28:43+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3542 Mtagusano wa Kimofofonolojia katika Kiolezofaridi cha Lugha ya Kiswahili: Mapengo ya Kiolezofaridi 2025-08-25T18:01:57+02:00 Naomi Ndumba Kimonye naomikimonye33@gmail.com Leonard Chacha Mwita chachamwita8@gmail.com Peter Githinji peter.githinji@ku.ac.ke <p>Makala hii inalenga kubainisha mapengo kwenye violezofaridi vya kimofofonolojia katika lugha ya Kiswahili. Kiolezofaridi ni mfumo wa mpangilio wa vipengee vya kiisimu ambao unaonyesha uhusiano wima baina ya kipashio kimoja na vipashio vingine katika muktadha maalum, yaani ni mfumo wa miundo ya kisarufi. Pengo la kimofofonolojia hutokea pale ambapo kipashio fulani cha lugha kinakubalika licha ya kuwa kimekiuka sheria&nbsp;&nbsp;&nbsp;&nbsp; za uundaji na mnyambuliko wa maneno. Pia hutokea pale ambapo hata baada ya kuzingatia sheria hizi tunapata kipashio ambacho hakikubaliki katika lugha. Katika utafiti huu, kuna maumbo yanayotii kanuni za kisarufi lakini hayakubaliki kiisimu ilhali kuna yale ambayo yamekaidi kaida za kisarufi lakini yanakubalika. Katika mofolojia, kanuni za kimofolojia zinapokiukwa katika uambishaji, tunatarajia kuwa maumbo yatakayozalishwa yatakuwa na makosa ya kisarufi na hivyo kutotumika. Kwa upande mwingine, maumbo ya lugha yanapokubalika licha ya kutozingatia kanuni za kimofolojia ni ishara kuwa kuna pengo la kiolezofaridi katika kiwango cha kimofolojia. Mofolojia hutagusana sana na michakato ya kifonolojia; hivyo basi katika makala hii tutashuhudia jinsi fonolojia inavyoathiri kiolezofaridi cha kimofolojia. Nadharia ya Kiolezofaridi Bora (Optimal Paradigms) iliyoasisiwa na McCarthy (2005) ndiyo iliyotumika. Misingi ya nadharia hii ni; kwanza, mshindani huzingatia vielelezo vya unyambuaji pale ambapo kiolezo cha unyambuaji huwa na maneno yaliyojikita kwenye msamiati mmoja. Pili, mashartizuizi ya uadilifu na uziada hutathmini washindani. Ukiukaji wa mashartizuizi wa kila kipashio hujumuishwa. Tatu, maumbotokeo hufanana na vielelezo vya vipashio vingine na hatimaye kuna makundi ya maumbotokeo ya mashartizuizi ya uadilifu yanayofanana. Data ya utafiti huu ilikusanywa maktabani na mtandaoni. Watafiti walisoma kwa kina vitabu vya lugha ya Kiswahili ambavyo vimechapishwa, tasnifu za lugha na pia, makala zilizochapishwa mtandaoni ili kupata data iliyohitajika. Asili ya data ni matini teule za isimu na data yenyewe ni violezofaridi vyenye mapengo. Usampulishaji dhamirifu ulitumika kuteua kazi za isimu. Data iliteuliwa kimakusudi na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo na majedwali. Matokeo ya utafiti huu yaliweka wazi kuwa mapengo katika lugha ya Kiswahili husababishwa na hali mbalimbali. Utafiti huu umebainisha kuwa katika lugha Kiswahili, mapengo ya violezofaridi yapo kwenye matawi ya fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki.</p> 2025-08-25T15:42:32+02:00 ##submission.copyrightStatement## https://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/3544 Mchango wa Ukafsiri katika Kukuza Isimu-Kokotozi: Mfano wa Nyimbo za Injili za Ambassadors of Christ na The Saints Ministers 2025-08-25T20:52:56+02:00 Ayub Oyimba Barasa ayubbarasa86@gmail.com John Kirimi M’raiji jmraiji@mmust.ac.ke Fred Simiyu Wanjala Wsimiyu@kibu.ac.ke <p>Ukafsiri ni taaluma muhimu katika tasnia ya isimu kokotozi ya Kiswahili na katika ufanikishaji wa mawasiliano. Aidha, taaluma ya ukafsiri inayohusu uhawilishaji wa ujumbe ama wa matini andishi kwenda mazungumzo. Au kutoka mazungumzo na kwenda katika maandishi. Imetekeleza jukumu hili la mawasiliano kwa njia ya kipekee kupitia Tehama. Katika karne hii ya 21, ukafsiri umetumia Teknolojia habari na mawasiliano (kuanzia sasa, Tehama) kama jukwaa la kutekeleza mawasiliano kwa umma mpana na kwa wakati mfupi iwezekanavyo. Aidha, lugha mbalimbali zimekuwa zikitumika na hata kutafsiriwa na zingine kukalimaniwa kwa lugha lengwa kwa minajili ya kufanikisha mawasiliano. Hii inaonesha kuwa kumekuwa na mshawasha wa kutaka kufikia idadi kubwa ya hadhira inayojua kusoma na isiyojua kusoma kwa lugha wanazozielewa. Makala hii inaongozwa na nadharia ya Ulinganifu Amilifu na ya Mawasiliano kutathmini nafasi ya Tehama katika kukuza na kuendeleza Kiswahili hasa katika Ukanda wa Afrika Mashariki huku ikijikita katika ukafsiri wa nyimbo za Ambassadors of Christ na The Saints Ministers zilizokafsiriwa kutoka Kiswahili hadi Kiingereza.&nbsp; Utafiti huu ulifamywa Maktabani. Upekuzi Wa vyanzo vya Utafiti pamoja na vitabu, kusikiza Kanda za video, tasnifu na wavuti na Kisha kuwasilisha kwa maelezo ya kinathari. Tehama ilisaidia kuondoa utata wa ulinganifu wa maana katika Matini chanzi kwenda Matini lengwa kwa kuambatanisha picha, kutumia fonti Tofautitofauti, alama za uakifishaji kama vile hisi, maswali ya balagha, lugha ishara na hata miondoko ya waimbaji ili kusaidia kukuza uelewa wa hadhira pokezi. Inatarajiwa kwamba utafiti utaongeza maarifa ya ukafsiri, usomaji na uhakiki wa kazi zilizokafsiriwa na kuwafaidi Wanafunzi, Wakafsiri, Walimu na Watafiti wa baadaye</p> 2025-08-25T00:00:00+02:00 ##submission.copyrightStatement##