Changamoto Zinazokumba Shirika la Utangazaji la Uganda Katika Kukikuza Kiswahili Jijini Kampala

  • Monday Geofrey Akol Chuo Kikuu cha Laikipia
  • Sheila Pamela Wandera-Simwa Chuo Kikuu cha Laikipia
  • James Onyango Ogola Chuo Kikuu cha Laikipia
Keywords: Changamoto, Shirika la Utangazaji, Kukikuza Kiswahili, Kampala
Sambaza Makala:

Ikisiri

Kiswahili nchini Uganda kimetumiwa tangu enzi za kabla ya ukoloni katika tasnia mbalimbali ila bado hakijaenea kama inavyostahili. Licha ya kuwa Uganda kuna sera, mazoea, na utaratibu wa kuendeleza Kiswahili, bado kina wakati mgumu kupenyeza kila mahali huku baadhi ya jamii ya Wanauganda wakibaki kuwa na mtazamo hasi kuhusu lugha hii adimu. Tafiti za awali zilionyesha kuwa mashirika ya utangazaji ya serikali ni muhimu sana katika kukuza lugha za mawasiliano ulimwenguni. Nchini Uganda, mtafiti hajakumbana na utafiti unaoonyesha chanagamoto zinazolikumba Shirika la Utangazaji la Uganda katika kukuza lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo utafiti huu ulinuia kutathmini changamoto zinazokumba Shirika la Utangazaji la Uganda katika kukikuza Kiswahili jijini Kampala. Utafiti ulitumia nadharia ya upangaji lugha kubaini hasa jinsi shirika hilo lenye vituo kumi na moja vya redio na vinne vya televisheni linavyokumbana na changamoto za kukuza Kiswahili katika jiji kuu la Kampala. Kwa kutumia nadharia hiyo utafiti uliegemea sana itikadi nne za upangaji lugha na vipengele vinne vya mchakato wa usanifishaji wa lugha hasa kile cha uimarishaji wa lugha. Mbinu za kurekodi, mahojiano, uchunzaji wa kushiriki na kusoma maktabani zilitumika katika kukusanya data. Sampuli ya utafiti huu kwa jumla ilihusisha watu 30 wakiwemo watumishi 20 wa Shirika la Utangazaji la Uganda ambapo 10 ni Waandishi Habari za Kiswahili. Watu 10 waliosalia waliteuliwa kutoka hadhira ya Shirika la Utangazaji la Uganda jijini Kampala. Utafiti huu uliwalenga wasikilizaji, watazamaji, watumishi wa makao makuu ya Shirika la Utangazaji Uganda jijini Kampala kwa vile wao ndio wadau waliochangia kwa kufanikisha madhumuni ya utafiti huu. Utafiti huu ulibainisha kuwa kuna wataalamu wachache katika lugha ya Kiswahili, ukosefu wa wahisani na ufadhili, kutokuwepo kwa sera madhubuti ya uhariri kuhusu Kiswahili, uhaba wa vitendea kazi na mitazamo hasi kwa lugha ya Kiswahili ni baadhi ya changamoto zinazokumba shirika la Utangazaji la Uganda katika harakati zake za kuendeleza lugha ya Kiswahili. Utafiti huu una manufaa kwa wizara zinazoshughulika na maendeleo ya Kiswahili Uganda kwa sababu vile utawapa mwanga kuhusu changamoto zinazolikumba Shirika la Utangazaji la Uganda katika harakati za kukukuza Kiswahili

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Ababaker E. (2013), Maendeleo ya lugha ya Kiswahili na Athari Zake kwa Jamii ya Kiarabu, Mtazamo wa kilughawiya Jamii. Tasnifu ya uzamifu katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Victor (2019), Language Planning in Higher Education. New York: Oxford University Press.

Kiango J. (2002), Nafasi ya Kiswahili Katika Ujenzi wa Jamii Mpya ya Afrika Mashariki, Swahili Forum Ix • 143—154

Miima, F. A. & Kawoya, V. F (2021). Msatakabala na Changamoto za Kiswahili Nchini Uganda. East African Journal of Swahili Studies, 3(1), 7077.https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.36.

Haugen, E. (1959), Planning for a standard language in modern Norway, Anthropological Linguistics 1(3). 8

King’ei, K, G. . (2000), Matatizo ya Matumizi ya Lugha Katika Vyombo vya Habari: Mifano Kutoka Kenya, AAP 64: Swahili Forum VII • 45-5

Haugen na Einar. (1959), Planning for a standard language in modern Norway, Anthropological Linguistics 1(3). 8

Mwesigye P. (2016) Report of the UBC Review Commission, Kampala, Shirika la Utangazaji la Uganda.

Ryanga na Ngowa (2018) Learning About language: An Introduction to Sociolinguistics. England: Edinburgh Gate.

Mwesigye (2016) Language and power: Longman. Google Scholar

Odawo M. and Onyango J. (2014). Kiswahili kama Chombo cha Kutangaza na Kuuza Vyombo vya Habari nchini Kenya. MULIKA Journal Number 35, 2016 Pg. 87 97.

Bamgbose A. (1991), Language and the nation, Edinburg. Edinburg, University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
9 Septemba, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Akol, M., Wandera-Simwa, S., & Ogola, J. (2024). Changamoto Zinazokumba Shirika la Utangazaji la Uganda Katika Kukikuza Kiswahili Jijini Kampala. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 393-404. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2200