Nafasi ya Mtindo Katika Utunzi wa Nyimbo Asili za Jamii ya Abagusii Kudhihirisha Ubabedume
الملخص
Utafiti huu ni sehemu ndogo ya utafiti wetu wa uzamifu ambao ulijikita kwenye mada Uchanganuzi wa Ubabedume katika Nyimbo Asili za Jamii ya Abagusii. Katika makala hii tumechambua namna mtindo umetumika katika nyimbo asili za jamii ya Abagusii kudhihirisha ubabedume. Katika utafiti huu tuliongozwa na nadharia ya Umtindo ambapo tulilenga kuchambua namna vipengele mbalimbali vya mtindo vimetumika katika utunzi wa nyimbo asili za jamii ya Abagusii kudhihirisha ubabedume. Tumeangazia baadhi ya vipengele vya kimtindo kama vile; tashbihi, maswali balagha, jazanda, usimulizi na takriri. Data za utafiti huu zilitokana na kusikiliza nyimbo asili kutoka kwenye mtandao wa Youtube, nyimbo asili alivyozirekodi Obuchi katika CD yake ya 2019. Tulizisikiliza kisha tukazinakili na kuzitafsiri kutoka lugha ya Ekehusii hadi lugha ya Kiswahili. Data nyingine muhimu zilitokana na usomaji wa tafiti zilizofanywa awali katika mada hii. Tulisoma tasnifu, majarida, vitabu na hata makala yaliyohusiana na mada hii. Mahojiano na wazee wa jamii ya Abagusii, wataalamu wa fasihi ya jamii ya Abagusii na wahadhiri wangu yalitufaa katika utafiti huu. Data ya utafiti huu ilichanganuliwa kwa mujibu wa lengo la utafiti huu tukiongozwa na mhimili wa nadharia ya umtindo unaosisitiza umuhimu wa vipengele vya fasihi kufumwa pamoja kupitia lugha ili kufanikisha mawasiliano. Uwasilishaji wa matokeo ya utafiti huu ulikuwa kupitia njia ya kithamano kwani ndiyo njia faavu zaidi ya kushughulikia mahusiano ya kijamii
التنزيلات
المراجع
Fadhili, E. F., (2014), Kuchunguza Dhima ya Mtindo Katika Tamthiliya za Kihistoria: Utafiti Linganishi wa Tamthilia za Morani na Kinjeketile. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. (Haijachapishwa )
Massoud, S. S., (2018), Kutathimini Matumizi ya Mtindo na Dhamira katika Tamthiliya za Mashetani na Mashetani Wamerudi: Utafiti Linganishi. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. (Haijachapishwa)
Mining, J. C., (2016), Mtindo katika Hadithi Fupi ya Kisasa ya Kiswahili. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa)
Muigai, M. N., (2024), Ubaadausasa kama Kunga ya Uandishi katika Riwaya za Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010) za Said Ahmed Mohamed na Unaitwa Nani (2008)? Ya Wamitila. Tasnifu ya Uzamifu. Chuo Kikuu cha Moi. (Haijachapishwa)
Mutungu, B. N., (2019), Taswira za Ulemavu Kama Mtindo katika Riwaya Teule za Said Ahmed Mohamed na Euphrase Kezilahabi. Tasnifu ya Uzamifu. Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa)
Mwongela, L. N., (2021), Usimulizi katika Riwaya ya Trilojia ya Kiswahili: Mfano wa Siri Sirini. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Chuka. (Haijachapishwa)
Nyutu, J. W., (2016), Mtindo katika Kazi za Kubuni za Leonard Sanja. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa)
Obuchi, J. B. M., (2019), Chingero Chi’Abagusii. Nairobi. A-Frame Publishers.
Obwogi, D. B., (2021), Mtindo katika Utenzi wa Vita vya Uhud. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa)
Oiko, F. G., (2017), Uhakiki wa Mtindo katika Tamthilia za Arege. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Maasai Mara. (Haijachapishwa)
Ongarora (2020), Usasa katika Ushairi wa Mberia: Tasnifu ya Uzamifu. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa)
Silavwe, M. L, (2016), Mtindo katika Riwaya ya Marimba ya Majaliwa ya Edwin Semzaba. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. (Haijachapishwa)
الحقوق الفكرية (c) 2024 Dickens Bonyi Obwogi, Stephen Oluoch, PhD, Riro Matinde, PhD, Ezra Nyakundi, PhD

هذا العمل مرخص حسب الرخصة Creative Commons Attribution 4.0 International License.