Mitindo ya Uwasilishaji wa Suala la Afya Katika Matini Teule za Fasihi ya Kiswahili ya Watoto

  • Reuben Mwilaria Chuo Kikuu cha Chuka
  • John Kobia, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
  • Dorcas Musyimi, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
##plugins.pubIds.doi.readerDisplayName##: https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2337
##share.article##:

Résumé

Fasihi ya Kiswahili ya Watoto ni mojawapo ya tanzu za fasihi ya Kiswahili inayotumiwa na wasanii kuhamasisha jamii kuhusu masuala yanayoiathiri kama vile magonjwa, uharibifu wa mazingira na ukiukaji wa haki za watoto miongoni mwa mengine. Zaidi ya hayo, madhara yanayotokana na changamoto za kiafya yamekuwa kikwazo katika maendeleo ya jamii na kuafikiwa kwa maendeleo endelevu katika mataifa mengi ulimwenguni. Kwa jinsi hii, makala hii ililenga kuchanganua mitindo ya uwasilishaji wa masuala ya kiafya yanayoathiri jamii na kutatiza kuafikiwa kwa maendeleo endelevu. Utafiti huu uliongozwa na malengo yafuatayo: Kuchunguza aina ya mitindo iliyotumiwa na waandishi wa matini teule kuwasilisha masuala ya kiafya, na kutathmini maana iliyowasilishwa na sitiari za kiafya katika mitindo ya uwasilishaji iliyotambuliwa katika matini teule. Matini zilizochanganuliwa katika kazi hii ni Madhila ya Bi. Shufaa (Bakari, 2016) na Kosa la Marehemu (Panja, 2010). Nadharia ya Umitindo iliyoasisiwa na Leech (1969) ili kuchunguza mitindo ya uwasilishaji wa kazi za kifasihi iliongoza utafiti huu. Aidha, uteuzi wa sampuli kimakusudi ulizingatiwa na data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuzingatia mkabala wa kimaelezo. Matokeo ya utafiti huu ni kuwa mitindo kama nyimbo, usimulizi na ushairi ilitumiwa kwa ufasaha kuwasilisha masuala ya kiafya katika matini teule. Vilevile, utafiti huu ulibainisha maana iliyowasilishwa na sitiari mbalimbali za kiafya zilizoangaziwa katika mitindo iliyotambuliwa. Uchunguzi zaidi ulipendekezwa kuhusu namna fasihi ya Kiswahili ya Watoto inavyoweza kutumiwa kidijitali kuangazia masuala ya kiafya yanayoathiri jamii. Hii ni kwa sababu mtindo wa kidijitali umeimarika sana kutokana na maendeleo ya kiteknolojia

##plugins.generic.usageStats.downloads##

##plugins.generic.usageStats.noStats##

Références

Akivaga, S.K. na Odaga, B. (1982). Oral Literature- A School Certificate Course. Nairobi: Heinemann.

Arege, M.T na Chacha, M.L. (2023). Kamusi ya Taaluma ya Kiswahili. Nairobi: Access Publishers Limited.

Bakari, N. (2016). Madhila ya Bi. Shufaa. Nairobi: Longhorn Publishers.

Bright, W. (1992). International Encyclopedia of Linguistics. New York: Oxford University Press. Bright, W. (1992). International Encyclopedia of Linguistics. New York: Oxford University Press.

Finnegan, R. (1970). Oral Literature in Africa. London: Oxford University Press.

Hunt, P. (1999). Understanding Children’s Literature: Key Essays from the International Companion Encyclopedia of Children’s Literature. New York: Routledge.

Indangasi, H. (1988). Stylistics. Nairobi: Nairobi University Press.

Kobia, J. (2008). Metaphor on HIV/AIDS Discourse Among Oluluyia Speakers of Western Kenya.http://cadaad.org/ejournal Vol 2 (2): 48-66 ISSN: 1752-3079. Kabira, W. M. na Mutahi, K. (1988). Gikuyu Oral Literature. Nairobi: Heinemann.

Kingei, K. & Ndalu, A. (2011). Kamusi ya Methali. Nairobi: East African Education Publishers

Leech, G. (1969). A Linguistic Guide to Engilsh Poetry. New York: Longman Group Ltd.

Leech, G. & Short, M. (1981). A Style in Fiction: An Introduction to English Fictional Prose. London: Longhorn.

Mbatiah, M. (2001). Kamusi ya Fasihi. Nairobi: Standard Textbooks Graghics and Publishing.

Mlaga, K.W. (2017). Misingi ya Ufundishaji na Ujifunzaji wa Fasihi Karne ya 21. Dar es Salaam: Heko Publishers.

Ngugi, P. (2014). Fasihi ya Watoto katika Kutekeleza Mahitaji ya Mtoto Kisaikolojia katika: Kiswahili Journal of the Institute of Kiswahili Studies vol. 77 (TATAKI). Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kur. 170-180.

Ngugi, P. (2016). Usawiri wa Masuala Ibuka katika Fasihi ya Watoto: Mifano kutoka Kenya katika: Mulika, No 35. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kur.76- 86.

Ngugi, P.M., & Nabea, W. (2011). Children’s Literature in Kiswahili: A Stylistic Approach katika: East African Literature: Essays on Written and Oral Traditions, Logos Verlag Berlin. Kur. 223- 244.

Mdee, J.S, Njogu, & K, Shafi, A. (2022). Kamusi Kuu ya Kiswahili (Toleo la Tatu). Nairobi: Longhorn Publishers PLC.

Nandwa, J. na Bukenya, A. (1983). Oral Literature for Schools. Nairobi: Longhorn.

Njogu, K., & Chimerah, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Panja, A. (2010). Kosa la Marehemu. Nairobi: Longhorn Publishers.

Senkoro, F.E.M.K. (1982). Fasihi. Dar es Salaam: Press and Publicity Centre.

Simala, K, I. (2000). Uhakiki wa Sitiari za Uana katika Ushairi wa Kiswahili. Tasnifu ya Uzamifu Chuo Kikuu cha Moi. (Haijachapishwa).

Timmamy, R. (2002). Mombasa Swahili Women’s Wedding Songs: A Stylistics Analysis. Tasnifu ya Uzamifu. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa).

Wamitila, K.W. (2008). Kanzi ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi wa Kiswahili. Nairobi: Vide – Muwa Publishers Lt d.

Wangari, M. (2019). Ukumbi wa Lugha na Fasihi: Mbinu za Sanaa katika Kiswahili. Available at https://taifaleo.nation.co.ke/ukumbi-wa-lugha-na-fasihi-mbinu-za sanaa-katika-kiswahili/: Accessed on 25/01/2022.

World Health Organization. (2018). The State of Health in the WHO African Region. An Analysis of the Status of Health, Health Services and Health Systems in the context of the Sustainable Development Goals. World Health Organization: Regional Office for Africa.

Publiée
24 octobre, 2024