Kuchambua Athari ya Vivumishi vya Runyakitara Katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili Nchini Uganda

  • Karuhanga Deusdedit Chuo Kikuu Cha Maseno
  • Indede Florence, PhD Chuo Kikuu Cha Maseno
  • Asiko Bevelyne Ambuyo, PhD Chuo Kikuu Cha Maseno
Keywords: Athari ya Vivumishi, Ujifunzaji wa Lugha, Uganda
Sambaza Makala:

Ikisiri

Katika mfumo wa elimu nchini Uganda, Kiswahili ni lugha muhimu kwa mawasiliano na maendeleo ya kijamii. Hata hivyo, wanafunzi wanaozungumza Runyakitara wanakumbana na changamoto katika kujifunza Kiswahili, hasa kwenye matumizi ya vivumishi. Tofauti za kimuundo kati ya vivumishi vya Runyakitara na Kiswahili huathiri uelewa sahihi wa Kiswahili, na mara nyingi uhamishaji wa vivumishi kutoka Runyakitara huleta makosa ya kiisimu. Wanafunzi ambao lugha yao ya kwanza ni Runyakitara hukumbana na matatizo wanapojifunza Kiswahili kama lugha ya pili. Utafiti huu ulilenga kuchunguza athari za vivumishi vya Runyakitara katika ujifunzaji wa Kiswahili kwa kubainisha tofauti za kimuundo, kuchunguza athari zake, na kutathmini makosa ya kiisimu yanayotokana na uhamishaji wa vivumishi hivyo. Utafiti huu uliendeshwa kwa mujibu wa nadharia ya uchanganuzi linganuzi, inayozingatia uingiliaji wa lugha ya kwanza, uhamishaji chanya na hasi, pamoja na utambulisho wa makosa. Utafiti ulifanyika Mbarara, Uganda, ukitumia mbinu ya usampulishaji nasibu na kimaksudi katika shule 10 na wanafunzi 100 wa Kiswahili wenye Runyakitara kama lugha ya kwanza. Data ilikusanywa kupitia mjarabu wa kimaandishi na kimazungumzo, na kuchanganuliwa kimaelezo kwa kutumia majedwali na michoro. Matokeo yalionyesha kuwa, ingawa Runyakitara na Kiswahili zinatoka nasaba moja, zina tofauti na mfanano katika matumizi ya vivumishi. Utafiti huu utakuwa na mchango mkubwa kwa wataalamu wa isimu, ukisaidia kuboresha matumizi sahihi ya Kiswahili sanifu na Runyakitara bila kusababisha mwingiliano hasi au kuibuka kwa lugha mseto

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Benedicto, J. (2021). A Comparative Analysis of Bantu Languages. Oxford University Press.

Bryman, A. (2016). Social Research Methods (5th ed.). Oxford University Press.

Chaudhary, A. (2022). Cross-linguistic Influence in Second Language Learning: A Contrastive Study. Language Learning Studies Journal, 14(2), 78-95.

Chebet, C. S. (2016). morphosyntactic analysis of Kinandi L1 speaking pupils’ Kiswahili essays as an insight into psycholinguistic challenges of second language acquisition (Tasnifu ya Uzamifu ya Chuo Kikuu cha Moi).

Chebet, C. S. (2016). morphosyntactic analysis of Kinandi L1 speaking pupils’ Kiswahili essays as an insight into psycholinguistic challenges of second language acquisition (Tasnifu ya Uzamifu ya Chuo Kikuu cha Moi).

Cohen, L., & Arieli, T. (2011). Research Methods in Education (7th ed.). Routledge.

Cohen, N., & Arieli, T. (2011). Field research in conflict environments: Methodological challenges and snowball sampling. Journal of Peace Research, 48(4), 423–435.

Egara, M.B (2016) Mofosintaksia ya Yambwa katika Kishazi cha Kiswahili. [Tasnifu ya uzamili], Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kenya.

Egera, A. (2016). Athari za Lugha ya Kwanza katika Ujifunzaji wa Lugha ya Pili. Jarida la Isimu ya Afrika Mashariki.

Fries, C. C. (1950). The Structure of English. Harcourt, Brace and Company.

Fries, C. C., & Lado, R. (1957). Linguistics Across Cultures: Applied Linguistics for Language Teachers. University of Michigan Press.

Fries, C. C., & Lado, R. (1957). Linguistics Across Cultures: Applied Linguistics for Language Teachers. University of Michigan Press.

Ghanen, (2005) The Child between Two Languages. In M. Karra, Second Language Acquisition: Learners’ Errors and ErrorCorrection in Language Teaching.Retrieved May 22, 2007 from http://www.proz.com/doc/633.

Gibson, H. & Taji, R (2018). The negative existential cycle in Bantu. Unpublished manuscript. University of Helsinki, Royal Museum of Central Africa, University of Essex.

Gibson, H., & Guérois, R. (2019). Variation in Bantu copula. The grammar of copulas across languages, 73, 213.

Guthrie, M. (2017). The Classification of the Bantu Languages bound with Bantu Word Division. Routledge.

Hamad Khamis, & Juma. (2015). NGELI ZA NOMINO ZA KI-MICHEWENI. Jarida La MULIKA Journal ., Juzuu la 3.

Hyman, L. M., & Katamba, F. X. (2012). 12 The syllable in Luganda phonology and morphology. In The Syllable (pp. 349-416). De Gruyter Mouton.

Hyman, L. M., na Katamba, F. X. (2001). November, 2001. Word Journal Of The International Linguistic Association, (L)

James, C. (1980). Contrastive Analysis. Longman.

Jarvis, S., & Pavlenko, A. (2019). Crosslinguistic Influence in Language and Cognition. Routledge.

Jean, M. (2022). Contemporary Language Learning Theories. Routledge.

Jerro, K. (2018). Linguistic complexity : A case study from Swahili. African linguistics on the prairie, 3(2018), 3–19. https://doi.org/10.5281/zenodo.1251708

Jilala, H. (2014). Athari za kiutamaduni katika tafsiri mifano kutoka matini za Kitalii katika makumbusho za Tanzania (Doctoral dissertation, University of Dar es Salaam).

Jjingo, C., & Visser, M. (2017). The Ssenteza Kajubi Legacy: The Promotion of Teaching Kiswahili in Uganda. Journal of Pan African Studies, 10(9).

Karuhanga. D na Beverlne Asiko A Uchanganuzi wa Makosa ya Kisarufi na athari zake katika matokeo ya Wanafunzi wa chuo kikuu cha Metropolitan. Metropolitan Journal of Social and Educational Research. Published in Vol.2 issue 4 July 2023.

Katamba, F. X. (2006). Uganda: The language situation.

Kombo, D. K., & Tromp, D. L. (2006). Proposal and Thesis Writing: An Introduction. Nairobi: Pauline Publications Africa.

Kothari, C. R. (2004). Research Methodology: Methods and Techniques (2nd ed.). New Delhi: New Age International Publishers.

Ladefoged, P. (2006). A Course in Phonetics (5th ed.). Boston: Thomson Wadsworth.

Masasa, J.I. (2017). Kuchunguza Athari ya vivumishi vya Lugha ya Runyakitara katika Ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili (Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu Huria, Tanzania).

Mdee J.S (2010) Nadharia na Historia ya leksikografia chupa ya tatu, DSM. Tuki

Mgullu (2005): Acquisition of English Syntax by Keiyo L1 Speak ers. Tasnifuya M.A (Isiyochapishwa), Chuo Kikuu cha Egerton, Kenya.

Milton Rwabushaija (2002) Kitabu cha chanza cha msingi wa Kiswahili. Fountain Publishers

Ntawiyanga, X. (2015). The Role of L1 in L2 Learning: Perspectives from Rural and Urban Classrooms. Kigali Academic Press.

Oduor, M., Inyani, B., na Kobia, J. (2017). Mwingiliano wa Lugha ya Kwanza katika Ujifunzaji wa Kiswahili. Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Philipo, Z. T. (2017). Tofauti Baina ya Vivumishi na Viambishi katika Lugha ya Kiswahili. Kioo cha Lugha, 13(1).

Richards, J. C., & Schmidt, R. (2002). Dictionary of Language Teaching and Applied Linguistics (3rd ed.). Harlow: Pearson Education.

Stern, H.H. (1983) Fundamental Concepts of Language Teaching. O.U.P, New York. The New Encyclopaedia Britannica, Vol. 4 Micropaedia (15 ed.). Encyclopaedia Bratannica Inc., Chicago, 1993.

Sundqvist, P., & Wikström, P. (2020). First Language Interference in Second Language Acquisition: The Role of L1 in L2 Learning. Language Acquisition Research Quarterly, 12(3), 134-153.

Tafida, A., & Okeke, C. (2021). The Role of Contrastive Analysis in Predicting Errors in Second Language Learning. African Journal of Applied Linguistics, 6(1), 56-70.

TUKI (2004) Kamusi ya Isimu na Lugha, Dar-es-salaam: Education Publishers and Distributors.

Tumwine, A. (2023). Teaching Kiswahili as a Second Language: Challenges and Solutions in Western Uganda. Education and Development Journal, 24(2), 62-78.

Van der Wal, D., & Namyalo, S. (2016). Language Acquisition in Multilingual Contexts: A Comparative Study of L1 and L2 Development in East Africa. Kampala Publishing House.

Wafula, K., & Njongu, R. (2007). Bilingual Education in Kenya: Challenges and Successes in L1 and L2 Integration. Nairobi University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
17 Novemba, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Deusdedit, K., Florence, I., & Ambuyo, A. (2024). Kuchambua Athari ya Vivumishi vya Runyakitara Katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili Nchini Uganda. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(2), 138-154. https://doi.org/10.37284/jammk.7.2.2420