Tathmini Ya Sura Za Ufisadi Katika Riwaya Za Tom Olali Mafamba (2012) Na Watu Wa Gehenna (2012)
Ikisiri
Utafiti huu unaeleza sura tofauti za ufisadi. Mtafiti amefanya hivi kwa kushughulikia riwaya ya Mafamba (Olali, 2012) na Watu Wa Gehenna (Olali, 2012). Ufisadi ni suala tata ulimwenguni na hata nchini Kenya. Dhana hii ni pana ila maelezo yake katika fasihi ni finyu kwa kuwa, msisitizo umekuwa kwenye usimamizi wa fedha za umma. Kulingana na Tume ya EACC (2016) kipengele cha IV, ufisadi unahusu unyanyasaji katika ofisi za umma, upendeleo, hongo, ulaghai, ukosefu wa uaminifu katika ofisi za umma, kutolipa ushuru au ada yoyote ile na kutofuata sheria zilizohidhinishwa kuteua viongozi katika ofisi za umma. Mtafiti ameangazia masuala hayo kwa kutathmini riwaya teule kwa lengo la kubainisha namna masuala hayo yalivyosawiriwa na kuleta uwezekano wa sura tofauti za ufisadi. Wahakiki kama vile; Muthumbi (2005) anaeleza ufisadi kama wizi wa pesa, Ochenga (2008) anaelezea ufisadi kama matumizi mabaya ya pesa za umma, Mayiek (2015) Ufisadi ni wizi wa mali ya umma, Sereti (2016) Ufisadi ni hali ya kujilimbikizia raslimali za taifa, Mwaniki (2018) Ufisadi ni unyakuzi wa mali ya umma.wahakiki hawa na wengineo wameeleza ufisadi kama matumizi mabaya ya fedha za umma na ndio sababu utafiti huu umeangazia sura tofauti za ufisadi. Riwaya zimeteuliwa kimakusudi na zimeangazia sura tofauti za ufisadi hivyo zilitupa data mwafaka. Nadharia ya Udenguzi ilitumika. Nadharia ya Udenguzi ilihusishwa na Jacques Derrida (1962).Waitifaki wake ni pamoja na Foocult, Roland Barthes, Jean Baudrillar, Paul Deman, J. Hills Miller, Jacques Lacan Barbara Johnstone na wengineo. Kupitia mihimili ya nadharia hii mtafiti alieleza fasiri mbalimbali za ufisadi. Utafiti huu ulifanywa maktabani kwa kusoma vitabu teule, tasnifu, majarida na makala ya mitandaoni yanayohusiana na mada. Data ya kimsingi ilitolewa kwenye riwaya teule. Data hiyo ilichanganuliwa kwa kuzingatia malengo na nadharia inayoongoza utafiti. Matokeo yamewasilishwa kwa kutumia njia ya maelezo. Utafiti huu utakuwa muhimu kwa wasomi na jamii kwa jumla hasa kwa kuagazia suala tata la ufisadi.
Upakuaji
Marejeleo
TUKI (2015). Kamusi kuu ya Kiswahili sanifu.Nairobi.Oxford university press.
Barthes, R. (1997). The death of the Author, in readings in the theory of religion. Routledge.
Derrida, J. (1976). Of grammatology and writting and diffrence. Routledge
Ethics and Anti-Corruption Commission. (2016). The Ethics and Anti-Corruption commission the fourth Quarterly report.
FOKUS, (2011). Kijitabu cha mwongozo wa kuzuia ufisadi.
Gasche, R. (1979). Deconstruction and Criticism. London: Routledge.
Kenya, L. O. (2013). The constitution of Kenya:2010. Chief Registrar of the judiciary Poe na Leech (1969). (Doctoral dissertation, Kenyatta University.)
Kimeu, A.N. (2016). Maudhui ya ukombozi katika wimbo mpya na msururu wa usaliti. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa).
Lomatoro, J. P. (2014). Viwango vya uhalisi na ubunifu katika riwaya teule za Kiswahili. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kiku cha Kenyatta. (Hajachapishwa).
Muthumbi, F. M. (2005). Mikakati na mbinu za usimilishwaji katika fasihi ya watoto. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).
Massawe, B. (2014). Kuchunguza masuala ya kisiasa katika riwaya za Shaaban Robert: Mfano wa Kusandikika na kufikirika. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha The Open, Tanzania. (Hajachapishwa).
Mayieka, M.N. (2015). Masuala ibuka katika riwaya za kisasa:Kidagaa kimemwozea na mhanga nafsi yangu. (Doctoral dissertation, Kenyatta university)
Mugenda, O.M., & Mugenda, A.G. (2003). Research Methods: Quantitative and qualitative approaches.(Vol. 2, No. 2). Nairobi: Acts Press
Mugwika, F.K. (2012). Dhana ya uchichimuzi katika uendelezaji wa Riwaya ya kimajaribio ya mafamba. (Doctoral dissertation, Nairobi University)
Muthui, E.K. (2019). Tathmini ya maudhui katika tamthilia teule za Kiswahili zinazotahiniwa shuleni za upili nchini Kenya: Mstahiki Meya (2009) na Kigogo (2016). (Doctoral dissertation, South Eastern University.)
Mutuku, K.M. (2016). Ukiushi katika tafsiri ya mashairi ya Kingereza: Mfano wa when the bullets begin to flower na risasi zianzapo kuchanua. (Doctoral dissertation, Kenyatta University.)
Miller, E.F. (1979). Metaphor and political knowledge. American Political Science Review 73,(1).155-170.
Mwaniki, J,M. (2018). Athari za mtagusano kati ya jamii na ekolojia katika ushairi wa Kithaka wa Mberia:Bara jingine na Rangi ya anga. (Doctoral dissertation, Nairobi University)
Njenga, A,W. (2021): Uongozi unavyojitokeza katika fasihi ya kisasa: Uchunguzi wa riwaya mpya ya miaka ya 2000. (Doctoral dissertation, Moi University.)
Ndung’u, B.W. (2022). Athari za matukio ya kihistoria katika riwaya za Nyongo Mkalia Ini na Mafamba.(Doctoral dissertation, Kenyatta University)
Njogu, K., & Chimera, R. (1999).Ufundishaji wa fasihi na mbinu.Jomo Kenyatta Foundation
Ochenga, R. (2008). Maigizo kama mbinu ya maudhui katika riwaya mbili za Ken Walibora.(Doctoral dissertation,Kenyatta University.)
Olali, T. (2012). Watu wa Gehenna. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.
Olali, T. (2012). Mafamba. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.
Ondoro, V.J. (2021). Maudhui ya siasa na athari zake katika jamii;mifano kutoka diwani ya kaza macho. (Doctoral dissertation, University of Nairobi)
Sereti, C. (2016). Taswira ya mwamko wa kisiasa miongoni mwa vijana katika tamthilia za Pango (2003) na Mstahiki Meya (2009). (Doctoral dissertation, Kenyatta University)
Wafula, R.M., & Njogu, K. (2007). Nadharia za uhakiki wa fasihi. Jomo Kenyatta Foundation.
Wamitila, K.W. (2003). Kamusi ya fasihi istilahi na nadharia.
Copyright (c) 2025 Pauline Musyoki, Jessee Murithi, PhD

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.