Kutumiya Alama za Kifasihi Kisiyasa ili Kušajiiša Mṭaji wa Kijamii: Kaďiya ya Sufi Ṁanalemba Kuvunja Upanga katika Uṭeṇḍi wa Siri Li Asrari

  • Mohamed Karama Chuo Kikuu cha Kabianga
  • Arthur Muhia Chuo Kikuu cha Pécs
  • Kineene wa Mutiso Chuo Kikuu Cha Nairobi
  • Rocha Chimerah Chuo Kikuu cha Pwani
Keywords: Siyasa, Ḍini, Sufi, Ṁanalemba, Kutumiya, Kutumiya Siyasa, Kuleta Siyasa, Mṭaji Kijamii
Sambaza Makala:

Ikisiri

Fasiri nyengine za kazi za kifasihi zapatikana k̇a kutiliya maanani mukṭaďa wa kihistoriya wa kazi hiyo. Fauka ya hayo, iṭikaḍiza kisiyasa, kiḍini, au kijinsiya ni miyongoni ṁa paradimu zinazoongoza muwonouliṁengu wa mtunzi wa kazi za kisanaa. Katika mfanyiko huu wa kučanganya masiyala ya kijamii na ya kiimani nripo uṭafiṭi wetu ulipoďamiriya kuuhakiki Uṭeṇḍi wa Siri li Asrari uliyotunġa ni Ṁanaṁarabu binṭi ḂanaLemba mnamo 1662 huko Paṭe, Kenya. Makala yetu yamejaribu kujibu maswali: mukṭaďa wa kihistoriya wa wakaṭi na mahali ulimšajiišaje mtunzi kuwasiliša ďamira yake k̇a mbinu ya kinahau? Je, ḍini, haswa ďehebu la kiSufi, iličangiyaje muwonouliṁengu wa mtunzi wakaṭi wa kuwasiliša alama za kiḍini katika kazi hiyo? Je, suluhišo la mtunzi kuhusu mukṭaďa wa siyasa ya wakaṭi huwo k̇a mkonro wa imani yake ulitatuwaje maafa ya wakaṭi huwo? Tuličanganuwa maṭini ya uṭeṇḍi huu tukiyongozwa ni naďariya ya uHistoriya Mpya k̇a k̇angaziya: alama, jazanra, ṭaswira, siṭiyara, kiyasi zilivotumiwa na mtunzi na aťari zake katika mfanyiko mzima wa kisiyasa. Data ya upili ilikusanywa ili tupate fasiri nyenginezo kuṭokana na mukṭaďa huwo k̇a sababu hayakujiṭokeza mayelezo haya katika uṭeṇḍi. Maṭokeyo yetu yanaďihiriša: k̇a kučanganuliwa luǧa ya nje kiyasi ya vita va Mtume Muhammaḍ (mhusika nguli) na Anďaruni (mhusika nruli) ilikuwa ni siṭiyara ya matukiyo ya wakaṭi huwo. Hali kaďalika, mtunzi ališajiišwa ni matukiyo hayo k̇enye uwasilišaji wake ambawo ulifasiri nahau za kusikiya siyasa (hisiya zake za mukṭaďa wa wakaṭi, mahali, na hali), k̇ingiliya siyasa (kuyazungumziya matukiyo), na kuleta siyasa (kukosowa kupita mipaka)—unukuďi wa msimamo wa aila yake ambao ni sosiyasa (maSufi hawaingii siyasani). Kinyumeče, data ilipočanganuliwa k̇a minaṭarafu ya luǧa ya nrani ya kifasihi ya kiSufi iliďihirika maana ya nahau kutumiya siyasa ni kutumiya hekima kuwaaiďi waumini wamṭegemee Mungu ṭu k̇a matatuzi ya matatizo yoṭʰe yanayowakabili hivo “kuvunja upanga” wa siyasa na kuweka imani k̇a Ṁenyezi Mungu. Uṭafiṭi wetu una naṭija ya kuwafafanuliya wanaluǧa umuhimu wa nahau za kiSwahili katika fasihi na haswa ikiwa nahau hizo zina aťari za uhasi kama lilivo neno siyasa leo

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abou-Bakr, O. (1992). The symbolic function of metaphor in medieval Sufi poetry: The case of Shushtari. Alif: Journal of Comparative Poetics 12, 40-57. https://www.jstor.org/stable/521635

Bang, A. K. (2003). Sufis and scholars of the sea: Family networks in east Africa, 1860-1925. RoutledgeCurzon.

Al-Beidh, M. S. S. (2011). Tarehe ya east Africa.pdf

Bertens, H. (2001). Literary theory: The basics. Routledge.

Biersteker, A. (1991). Language poetry and power: A consideration of “Utendi wa Mwanakupona”. Katika K. W. Harrow (mh.) Faces of Islam in African literature, 59—78. Heinamann Educational Books.

Boxer, C. R. and Azevedo, C. (1960). Fort Jesus and the Portuguese in Mombasa. Hollis and Carter.

Bujra, A. S. (2017). Conclusion: Research issues concerning Hadhramaut. Katika N. Brehony (mh.), Hadhramaut and its diaspora Yemeni politics, identity and migration, kur. 225—232. I. B. Tauris.

Buturovic, A. (1996). Spiritual empowerment through spiritual submission Sufi women and their quest for God. Canadian Women Studies, 17 (1), 53—56.

Dammann, P. E. (1940). Dichtungen in der Lamu mundart des Suaheli Band 28. Freiderichesen.

Al-Ghazali, H. (1952). Deliverance from error and attachment to the Lord of Might and Majesty. Imetafsiriwa na Montgomery Watt. George Allen and Unwin Ltd.

Gulen, M. F. (2011). Emerald hills of the heart: Key concepts in the practice of Sufism 2. Tughra Books.

Al-Hakim, S. (1981). Mu’jam AlSufi (Sufi Lexicon) (1st ed.). Dar Nadrah for Printing and Publishing.

Hanieh, H. (2011). Sufism and Sufi orders: God’s spiritual paths adaptation and renewal in the context of modernization. Friedrich-Ebert-Stiftung.

Hennink, M., Kiiti, N., Pillinger, M & Jayakaran, R. (2012). Defining empowerment: Perspectives from international development organisations. Development in Practice 22 (2), 202—215. http://dx.doi.org/10.1080/09614524.2012.640987

Heywood, A. (2013). Politics (4th ed.). Palgrave Macmillan.

Karama, M. (2018). Maana timilifu kutokana na undimi katika utendi wa siri li asrari. Tasnifu ya Uzamifu (Haijachapishwa), Pwani University, Kilifi.

Karama, M., Chimerah, R., na wa Mutiso, K. (2018). Ushairi wa kiSufi katika tendi za kale za Kiswahili: Mfano wa utendi wa siri li asrari. Mara res. j. Kiswahili 3 (1), 1 – 9.

Karama, M., Chimerah, R. & Kineene, M. (2021). Si t̪end̪i zot̪ʰe za kabla ya karne ya ishirini ni utambaji wa kingano nyengine ni ufunzaji: Kiyelelezo cha ut̪end̪i wa siri li asrari. East African Journal of Swahili Studies, 3(1), 51-57. https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.349.

Knappert, J. (1979). Myths and legends of the Swahili. East African Educational Publishers.

Knappert. J. (1988). Four centuries of Swahili verse: A literary history and anthology. Darf Publishers Limited.

Lee, J. A. B. (2001). The empowerment approach to social work practice building the beloved community (2nd ed.). Columbia University Press.

Madan, A. C. (1903). Swahili - English dictionary. Clarendon Press.

Martin, C. M. P. & Martin, E. B. (1973). Quest for the past: An historical guide to the Lamu archipelago. Marketing and Publishing Limited.

Mlamali, M. (1980). Al Inkishafi: Ikisiri ya Mlamali. Longman Kenya.

Muhammad, Y. K. (2003). Almausuatu alyusufiyah fi bayani adillah alSufiyah (The Yusufiya encyclopedia in explaining the evidence of Sufism). Daru Taqwa.

Mulokozi, M. M. & Sengo, T. S. Y. (2005). History of Kiswahili poetry A.D. 1000 - 2000. Institute of Kiswahili Research.

Mustafa, I. (2004). Mu’jam Al Wasit (Intermediate dictionary) (4th ed). Al-Shorouk National Library.

Wa Mutiso, K. (2003). Utenzi wa siri li asirali [afuan] with a translation in English. Mswada haujachapishwa. Kanzi ya Profesa Kineene wa Mutiso.

Wa Mutiso, K. (2014). Number symbolism in world religions: The case of number seven. Journal of Oriental and African Studies, 23, 405-415.

Ndzovu, H. J. (2014). Muslims in Kenyan politics political involvement, marginalization, and minority status. Northwestern University Press.

Perkins, D. D. & Zimmerman, M. A. (1995). Empowerment theory, research, and application. American Journal of Community Psychology 23 (5), 569—579.

Perkins, D. D. (2010). Empowerment. Katika R.A. Couto (mh.), Political and civic leadership: A reference handbook, kur. 207-218. Thousand Oaks.

Rom, M. C., Hidaka, M. & Walker, R. B. (2022). Introduction to political science. OpenStax.

Roskin, M. G., Cord, R. L., Medeiros, J. A., Jones, W. S. (2012). Political science: An introduction (12th ed.). Longman.

Rumman, M. (2020). Mysteries of the Sufi path: The Sufi community in Jordan and its zawiyas, hadras and orders. Friedrich-Ebert-Stiftung.

Sameja, M.A. (h.t.). Aali Ba Alawiy: Sehemu ya kwanza.pdf

Schimmel, A. (1975). Mystical dimensions of Islam. The University of North Carolina Press.

Schimmel, A. (1982). As through a veil: Mystical poetry in Islam. Columbia University Press.

Sell, T.M. (2023). An introduction to politics. Libretexts.

Shariff, I. N. (1988). Tungo zetu: Msingi wa mashairi na tungo nyenginezo. The Red Sea Press.

Sheriff, A. (2002). Slaves, spices, & ivory in Zanzibar: Integration of an east African commercial empire into the world economy, 1770-1873. East African Educational Publishers.

Wa Thiong’o, N. (1994). Writers in politics: Essays. East African Educational Publishers.

Wa Thiong’o, N. (2016). Abdilatif Abdalla and the voice of prophecy. Katika R. M. Beck & K. Kresse (wah.), Abdilatif Abdalla: Poet in politics. Mkuki na Nyota Publishers Limited. 11—18.

Tindall, W. Y. (1955). The literary symbol. Columbia University Press.

Van Deth, J. W. (2021). What Is Political Participation? DOI:10.1093/acrefore/9780190228637.013.68

Walker, I. (2017). Citizenship and belonging among the Hadhramis of Kenya. Katika N. Brehony (mh.), Hadhramaut and its diaspora Yemeni politics, identity and migration, kur. 164—182. I. B. Tauris.

Wikipedia.org. https://en.m.wikipedia.org/wiki/George_Eliot

Wilde, D. (h.t.). On Sufism and Poetry. http://www.unc.edu/depts/Sufilit/Wilde.html

Tarehe ya Uchapishaji
12 Machi, 2025
Jinsi ya Kunukuu
Karama, M., Muhia, A., wa Mutiso, K., & Chimerah, R. (2025). Kutumiya Alama za Kifasihi Kisiyasa ili Kušajiiša Mṭaji wa Kijamii: Kaďiya ya Sufi Ṁanalemba Kuvunja Upanga katika Uṭeṇḍi wa Siri Li Asrari. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 8(1), 201-215. https://doi.org/10.37284/jammk.8.1.2760

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.