Mbinu za Lugha Katila Ujenzi wa Ujitambuzinafsia wa Jinsia na Upembezwaji wa Mwanamke katika baadhi ya Bunilizi za Clara Momanyi na Omar Babu

  • Kawira Kamwara Chuo Kikuu cha Mount Kenya
Keywords: Ujitambuzinafsia, Upembezwaji, Mbinu za lugha, Ubaada wa Ufeministi wa Kiafrika, Bunilizi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Jamii nyingi za Kiafrika ni za kuumeni na humpembeza mwanamke kwa kumweka katika ngazi za chini akilinganishwa na mwanamume. Upembezwaji wa mwanamke katika tungo za kifasihi na katika maendeleo ya jamii ni matokeo ya mwingiliano wa fahamu tambuzi na fahamu bwete za mtunzi hasa kwa mujibu wa utamaduni wa jamii lengwa. Mwingiliano huu wa ufahamu tambuzi na ufahamu bwete unaekezwa kwa makusudi katika utunzi wa tungo mahususi kama ilivyo kwenye tungo za Momanyi ‘Ngome ya Nafsi’ katika Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine (2004), Tumaini (2006) na Nakuruto (2010)  nazo za Babu ni Kala Tufaha (2007), Heri Subira (2010) na ‘Ndoa ya Samani’ (2011). Nadharia tuliyotumia ni ya Ubaada wa Ufeministi wa Kiafrika iliyoasisiwa na Steady (1981). Mwanaufeministi huyu alisema kuwa Ubaada wa Ufeministi wa Kiafrika huweka masuala pamoja ya kijinsia, ubaguzi, mielekeo ya kiutamaduni na tabaka ili kumwangalia mwanamke kama kiumbe mtegamewa bali sio mtegemezi. Data ya usomi huu ilitokana na usomaji wa bunilizi hizi maktabani. Tuliweza vilevile kutumia mitandao kurutubisha utafiti wetu. Hivyo, ni kwa jinsi gani lugha ilivyosukwa kiusanii kujenga ujitambuzinafsia wa kijinsia na upembezwaji wa mwanamke kwenye tungo za waandishi hawa wawili? Je, mbinu teule za lugha zinakuza mtazamo upi wa kijinsia kwenye tungo hizi? Je, kuna mfanano au tofauti katika matumizi ya mbinu za lugha kwenye kazi za watunzi hawa?  Maswali haya ndiyo tulipania kuyajibu katika makala haya

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Babu, O. (2007). Kala Tufaha. Nairobi: Oxford Publishers.

Babu, O. (2010). Heri Subira. Nairobi: Oxford Publishers.

Bank, O. (1990). Faces of Feminism. A study of Feminism as a Social Movement. Basil Blackwell: USA.

Chacha, W. C. (2013). ‘Taswira ya mwanamke katika tamthilia za Nguzo Mama na Mama Ee’. Tasnifu ya Umahiri, Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapioshwa.)

Chesaina, C. (1987). ‘Women in African Drama: Representation and Role’. Tasnifu ya Uzamifu, University of Leeds. (Haijachapishwa).

Kamwara, K., (2022). ‘Ujenzi wa Ujitambuzinafsia wa Jinsia na Upembezwaji wa Mwanamke katika Bunilizi za Clara Momanyi na Omar Babu. Tasnifu ya Uzamifu Chuo Kikuu cha Nairobi, (Haijachapishwa

Kamwara, K., (2016). ‘Mtazamo Mpya katika Sauti ya Kike katika Riwaya ya Kiswahili’. Tasnifu ya Uzamili Chuo Kikuu cha Mount Kenya. (Haijachapishwa).

Mbatiah, M. (2001). Kamusi ya Fasihi na Nadharia. Nairobi: Standard Text Books Graphics and Publishing.

Mboya, L. A., Mohochi, E. S., & Kisurulia, S. (2018). ‘Dhuluma kama Kichocheo cha Mzinduko wa Wanawake katika Riwaya ya Kiswahili’. Rongo: Rongo University Press. (http://respository.rongovasity.ac.ke/handle/123456789/1860).

Mikell, G., (1997). African Feminism: The Politics of Survival in Sub-Sahara Africa. Mji? University of Pennsylvania Press.

Mohochi S., et. (2018). ‘Dhuluma kama Kichocheo cha Mzinduko wa Mwanamke katika Riwaya ya Kiswahili’. Makala ya Chuo Kikuu Cha Rongo.

Musyoka F. M. (2011). ‘An Analysis of the Woman in Gender Role-Play Dynamics in Kenyan Kiswahili Drama.’ Tasnifu ya Umahiri. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa.)

Hamadi, M. (9.7.2019). ‘Mwanamke Bomba’ (Msururu wa Vipindi vya Televisheni vya ‘Citizen Kenya”). (https://youtu.be/FrBDtjx_SM).

Nation. Africa 4.11.2011. “Wambui and Mbugua Cap Marriage with Church Wedding. (https://nation.africa/kenya/news/mambui-and-mbugua-cap-marriga-with-hurch-wedding--755458).

Njogu, K. na R. Chimerah (1999). Ufundishaji Wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Pinkie, M., (2006). ‘Theorizing African Feminism(s): The Colonial Question.’ QUEST: An African Journal of Philosophy vol. 20 (1-2): 11-22.

Steady, F.C. (2005). ‘An Investigative Framework for Gender Research in Africa in the New Millennium katika. African Gender Studies: A Reader. (pp. 313-331). New York: Palgrave Macmillan,

Swaleh, A. (2011). ‘A Critique of the Mapping and Construction of Gender Identity and Authority in Selected Kiswahili Novels’. Tasnifu ya Umahiri. Chuo Kikuu cha Nairobi.

Wafula, R. M. na K. wa Njogu (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Wamitila, K. W. (2002). Uhakiki wa Fasihi; Nadharia na Mbinu. Nairobi: Phoenix Publishers.

Wamitila, K. W. (2003). Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Publishers.

Tarehe ya Uchapishaji
17 April, 2025
Jinsi ya Kunukuu
Kamwara, K. (2025). Mbinu za Lugha Katila Ujenzi wa Ujitambuzinafsia wa Jinsia na Upembezwaji wa Mwanamke katika baadhi ya Bunilizi za Clara Momanyi na Omar Babu. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 8(1), 250-264. https://doi.org/10.37284/jammk.8.1.2883