Jinsia ya Mtunzi na Usawiri wa Wahusika katika Riwaya za Kiswahili: Nyuso za Mwanamke na Nguu za Jadi

  • Mary Nyambura Mwangi Chuo Kikuu cha Mount Kenya
  • Kawira Kamwara Chuo Kikuu cha Mount Kenya
Keywords: Chanya, Hasi, Jinsia, Kweza, Tweza, Usawiri, Ubabedume, Wahusika
Sambaza Makala:

Ikisiri

Kila mwandishi huathiriwa na sababu mbalimbali katika usawiri wa wahusika kwenye utunzi wake. Ni kwa sababu hii basi tumeweza kuchunguza athari ya jinsia ya mwandishi katika usawiri wa wahusika katika riwaya za Kiswahili. Tumeweza kubainisha jinsi usawiri wa wahusika katika riwaya huathiriwa na jinsia ya mwandishi. Hii ni kwa sababu kuwa wahusika katika riwaya huwa wengi na husawiriwa kwa njia mbalimbali. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni nadharia ya Ufeministi wa Kiafrka iliyoasisiwa na Steady (1981). Utafiti huu ulifanyika maktabani. Data ilikusanywa kupitia usampulishaji lengwa kutoka katika riwaya teule ambazo ni; Nyuso za Mwanamke (2010) Said A Mohamed na Nguu za Jadi (2021) Clara Momanyi. Data hii imechanganuliwa kwa njia ya maelezo kwa mujibu wa malengo ya utafiti na mihimili ya nadharia teule. Utafiti huu utawafaidi wasomi, watafiti na wahakiki wa kazi za kifasihi kwa kuwa utachangia kujaza mapengo katika utafiti hasa kuhusu masuala ya kijinsia. Vilevile, tumekusudia utafiti huu uweze kuwafaidi wahakiki na wasomi katika kuzitafiti kazi nyinginezo za kifasihi. Mbali na hayo, utafiti wetu utatumika kama marejeleo kwa watafiti wa masuala ya kijinsia wa siku zijazo katika uendelezaji wa tafiti zao. Jinsia ya mtunzi inaathiri vipi usawiri wa wahusika ? Mwanamke anasawiriwa vipi katika kazi za watunzi hawa ? Je, mwanmke anaonyesha mtazamo upi wa maisha yake kisaniii katika jamii ? Haya ndiyo maswali tunapania kujibu katika utafiti huu

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Chesaina, C. (1987). Women in African Drama.Tasnifu ya PhD.Chuo Kikuu Cha Leeds.

Lugano, R. S. (1989). Mwanamke katika Riwaya ya Kezilahabi: Tasnifu ya M.A Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa)

Momanyi, C (2021). Nguu za Jadi.Nairobi: Queenex Publishers Limited.

Millet, K. (1969). Sexual Politics.London: Virago press.

Said, A. M. (2010). Nyuso za Mwanamke.Nairobi. Longhorn publishers.

Steady, F. C. (1981). Black Women Cross Culturally. Cambridge: Mass Scherkman Publishing Co.Inc.

Ogundipe-Leslie, O. (1994): “African Women, and Critical Transformations; Trenton African World Press.

Wamitila, K. W. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Nairobi.Phoenix Publisher.

Tarehe ya Uchapishaji
12 June, 2025
Jinsi ya Kunukuu
Mwangi, M., & Kamwara, K. (2025). Jinsia ya Mtunzi na Usawiri wa Wahusika katika Riwaya za Kiswahili: Nyuso za Mwanamke na Nguu za Jadi. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 8(1), 410-423. https://doi.org/10.37284/jammk.8.1.3131