Vichocheo Vinavyowafanya Wahudumu wa Bodaboda na Abiria Kuzingatia au Kukiuka Upole Katika Mawasiliano
Ikisiri
Upole ni muhimu katika kufanikisha mawasiliano. Husaidia katika kukabiliana na matendo ya kutishia uso. Utafiti huu ulilenga kuchunguza kuhusu sababu zinazowachochea wahudumu wa bodaboda na abiria kuzingatia au kukiuka matumizi ya mikakati ya upole katika mawasiliano yao. Nadharia ya upole ndiyo iliyotumika kuelekeza utafiti huu. Utafiti ulifanyika katika kaunti ndogo ya Mbooni iliyo katika kaunti ya Makueni, nchini Kenya. Walengwa walikuwa ni wahudumu wa bodaboda na abiria walioteuliwa kimakusudi hadi pale ambapo kiwango kifu kilifikiwa. Utafiti huu wa kithamano, ulitumia mbinu ya uchunzaji na mahojiano katika kukusanya data. Uchanganuzi wa kimaudhui ulitumika ili kuhakiki majibu ya mahojiano kwa kuelekezwa na mihimili ya nadharia. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa kuna sababu kadhaa zinazochochea hali ya kuzingatia au kukiuka matumizi ya mikakati ya upole katika mawasiliano. Sababu hizo ni kama vile: faida tarajiwa, tofauti za mahusiano, haja ya kutaka kuonyesha heshima kwa sababu ya tofauti za kimamlaka na hali ya kutaka kukabiliana na uzito wa tendo la kutishia uso. Faida au matokeo tarajiwa yalichochea uzingatiaji wa mikakati ya upole sana. Sababu hii ilijitokeza kwa wingi kwani mawasiliano yalitokea katika muktadha wa uchukuzi ambapo mantiki huzingatiwa sana ili kufikia malengo ya kibiashara. Hivyo, wahudumu wa bodaboda na abiria walizingatia zaidi mafanikio ya mawasiliano kuliko vipengele vya kijamii. Matokeo ya utafiti huu yanaiarifu nadharia kwani yanaonyesha kuwa mbali na vigezo vya kijamii vinavyosisitizwa na nadharia, faida tarajiwa huchochea matumizi ya mikakati ya upole katika muktadha wa uchukuzi. Utafiti huu una umuhimu kwa taaluma ya mawasiliano hasa kwa kurahisisha maingiliano baina ya watu katika jamii. Isitoshe utakuwa wenzo muhimu kwa watafiti wa baadaye watakaojihusisha na uga wa pragmatiki
Upakuaji
Marejeleo
AlShlowi, A. H. (2023). An Analysis of Politeness Strategies used by Non-Native Saudi English Speakers in Family Gatherings. Journal of English Language Teaching and Applied Linguistics, 5(2), 15–24. https://doi.org/10.32996/jeltal.2023.5.2.2
Anuonye, F. D. (2018). Politeness Strategies in Conversational Discourse as a Panacea for Emerging Conflict. Interdisciplinary Journal of African & Asian Studies, 1(4), 1–9.
Aririguzoh, S. (2022). Communication competencies, culture and SDGs: effective processes to cross-cultural communication. Humanities and Social Sciences Communications, 9(1), 1–11.
Ascigil, E., Gunaydin, G., Selcuk, E., Sandstrom, G. M., & Aydin, E. (2025). Minimal Social Interactions and Life Satisfaction: The Role of Greeting, Thanking, and Conversing. Social Psychological and Personality Science, 16(2), 202–213. https://doi.org/10.1177/19485506231209793
Brown, P., & Levinson, S. (1987). Politeness: Some Universals in Language Usage. Cambrigde University Press, 345.
Culpeper, J. (2011). Politeness and impoliteness. Pragmatics of Society, 5, 393–438.
Dahl, A. (2023). What We Do When We Define Morality (and Why We Need to Do It). Psychological Inquiry, 34(2), 53–79. https://doi.org/10.1080/1047840X.2023.2248854
Daulay, S. H., Azmi, N., & Pratiwi, T. (2022). The Importance of Expressing Politeness: English Education Student’s Perspectives. Tarling : Journal of Language Education, 6(1), 49–68.
Dirgantara, B. G., & Gunawan, H. (2024). The Usage of Greetings Varieties at Widyatama Campus Environment: A Sociolinguistics Study. JL3T (Journal of Linguistics, Literature and Language Teaching), 10(1), 80–95. https://doi.org/10.32505/jl3t.v10i1.8047
Duevel, C. (2019). SAGE Research Methods. The Charleston Advisor, 19(4), 38–41.
Fitriyani, S., & Andriyanti, E. (2020). Teacher and Students’ Politeness Strategies in EFL Classroom Interactions. IJELTAL (Indonesian Journal of English Language Teaching and Applied Linguistics), 4(2), 259.
Gross, J., & Vostroknutov, A. (2022). Why do people follow social norms? Current Opinion in Psychology, 44, 1–6.
Hamood, B., & Challob, A. (2023). Age Impact on the Use of Politeness Strategies in Online Interaction by EFL Students in Al-Anbar Distinguished School for Girls. Al-Adab Journal, 145, 43–52. https://doi.org/10.31973/aj.v2i145.4195
Haryanto, H., Indriani, N., Safar, M., Fansiska, F. W., & Dewi, D. U. (2024). The Use of Politeness Strategy and The Influence Factors in Political Talk Show. Surakarta English and Literature Journal, 7(1), 86–100.
Hassan, H., Mohd. Sapuan, W. N., Azmimurad, A. M., & Rostam, N. L. S. (2022). The Employment of Language Politeness Strategies in Student-Lecturer Virtual Interaction. International Journal of Academic Research in Business and Social Sciences, 12(11), 2826–2836. https://doi.org/10.6007/ijarbss/v12-i11/15372
Kioko, N. (2021). Mikakati ya Upole Katika Mawasiliano ya Wahudumu wa Magari ya Uchukuzi na Abiria katika lugha ya Kikamba. Editon Consortium Journal of Kiswahili, 3(1).
Knott, E., Rao, A. H., Summers, K., & Teeger, C. (2022). Interviews in the social sciences. Nature Reviews Methods Primers, 2(1), 1–36.
Korta, K. (2008). Malinowski and pragmatics. Claim making in the history of linguistics. Journal of Pragmatics, 40(10), 1645–1660.
Machira S. (2015). Uchambuzi wa mikakati ya upole kama inavyotumiwa na wahusika wakuu katika tamthilia ya Mbaya Wetu. Chuo Kikuu cha Nairobi.
Magashi, S. (2023). The role of address terms in expressing politeness in social interaction in Sukuma. Journal of Linguistics and Language in Education, 17(2), 107–135. https://doi.org/10.56279/jlle.v17i2.5
Mapunda, G., & Sommer, G. (2017). When Shikamoo Mama/Baba replaces Tukuwoni Mawu/Dadi: An account of shifting access rituals among the Ngoni of Tanzania. Linguistik Online, 84(5).
Mosha, E. S. (2023). Matumizi ya sitiari katika kazi za fasihi: Mifano kutoka nyimbo za kivunjo. Kioo Cha Lugha, 20(1), 18–35. https://doi.org/10.4314/kcl.v20i1.2
Mwangi, R. M. (2024). Influence of Entrepreneurial Opportunities and the Growth Sustainability of Motorcycle ( Boda-Boda ) Industry for Economic Development in Murang’a County, Kenya. 4(4), 1–13.
Nashruddin, N., Alam, F. A., & Harun, A. (2020). Moral Values Found in Linguistic Politeness Patterns of Bugis Society. Edumaspul: Jurnal Pendidikan, 4(1), 132–141. https://doi.org/10.33487/edumaspul.v4i1.340
Nyambwogi, J. M. (2016). Mikakati ya Upole na Uana: Tathmini ya Natala. Chuo Kikuu cha Nairobi.
Obidovna, D. Z. (2022). the Main Concepts of Politeness in Modern Linguopragmatics: the Politeness Principle By J. Leech. International Journal of Pedagogics, 02(11), 16–17.
Olorunsogo, D. (2020). Pilot study: Politeness Strategies in Selected Doctor- Patient Interactions in Ibandan Private Hospitals. International Journal of Research and Innovation in Social Science (IJRISS), IV(VIII), 2454–6186.
Pang, H. (2022). The investigation of politeness strategies in teacher-student interactions : The use of the Michigan corpus of academic spoken English. Journal of Communication in Scientific Inquiry (JCSI), 4(1), 1–14.
Sembiring, E. M., Simanjuntak, F. M. P., Tarigan, K. J., & Silalahi, V. (2023). Politeness in the EFL Classroom Interaction: Strategies in Avoiding Face Threatening Act (FTA). Journal of Classroom Action Research, 1(2), 18–26. https://doi.org/10.52622/jcar.v1i2.73
Simon, J. (2014). Three case studies. Education and Training in Solution-Focused Brief Therapy, 149–154.
Stephan E, L. N. (2010). Politeness and Psychological Distance: A Construal Level Perspective. J Pers Soc Psychol., 98(2), 268–280. https://doi.org/10.1037/a0016960.Politeness
Taylor, S., Simpson, J., & Hardy, C. (2022). The Use of Humor in Employee-to-Employee Workplace Communication: A Systematic Review With Thematic Synthesis. International Journal of Business Communication. https://doi.org/10.1177/23294884211069966
Thanh, P. T. K., Ngoc, D. T., An, L. T., Thu, N. T. T., & Huong, L. D. T. (2022). Types of Politeness Strategies and Degrees of Politeness Performed By English Major Students in Requesting for Help. European Journal of Education Studies, 9(12), 90–118.
Tiryakian, E. A., & Goffman, E. (1967). Interaction Ritual: Essays on Face-to-Face Behavior. American Sociological Review, 33(3), 462.
Trávníková, P. (2012). Building Rapport in an Online Community Via Positive Politeness Strategies. Discourse and Interaction, 5(2), 67. https://doi.org/10.5817/di2012-2-67
van Dijk, T. A. (2021). Epistemic context analysis. Revista Signos, 54(107), 758–770. https://doi.org/10.4067/S0718-09342021000300758
Wafula, M. (2019). Mikakati ya Utoupole katika Tamthiliya ya Pango ya Kyallo Wadi Wamiila. Chuo Kikuu cha Nairobi.
Waziri, Z. Y. (2022). Politeness Theory and Resolution of Misunderstandings in Social Media Communication. Nsukka Journal of the Humanities, 30(2), 61–70. https://doi.org/10.62250/nsuk.2022.30.2.61-70
Copyright (c) 2025 Faith Mbithe Kathukya, John Khaisie Wanyama, PhD, Timothy Kinoti M’ngaruthi, PhD

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.