Mikakati ya Kimtindo katika Muziki wa Benga wa Jamii ya Wakamba: Mkabala wa Umtindo
Ikisiri
Muziki wa benga ni utanzu maarufu nchini Kenya. Hujitambulisha kwa sifa ya mdundo na mapigo ya kasi pamoja na ustadi wa msanii wa kucheza gitaa na kuimba kwa mtindo maalum. Utafiti huu ulilenga kubainisha mikakati ya mtindo inayotumika katika muziki wa benga wa jamii ya Wakamba kujenga hisia na athari za kijamii. Uchunguzi huu uliongozwa na kielelezo cha Umtindo. Umtindo hufasiri na kuhakiki tungo kwa kuzingatia mtazamo wa kiisimu kama taaluma iliyo na uhusiano wa karibu na fasihi. Uchunguzi wa kimtindo huhusisha namna lugha inavyotumika katika matini ili kujenga maana na athari. Usampulishaji ulifanywa kimakusudi ambapo nyimbo tano za muziki wa benga wa jamii ya Wakamba ziliteuliwa. Ukusanyaji wa data ulihusisha upakuaji wa nyimbo za benga kutoka kwa mtandao wa kijamii wa Youtube na unakili wa mishororo yake. Mbinu ya uchanganuzi matini ilitumika kubainisha mikakati ya kimtindo na kuchanganuliwa kithamano kwa kuelekezwa na mihimili ya nadharia ya umtindo. Data zilikuwa ni maneno, dhana, kauli, virai na sentensi zinazotumiwa na waimbaji wa muziki wa benga wa jamii ya Wakamba zinazohusisha vipengele vya kimtindo. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kimaelezo. Ilibainika kuwa, waimbaji wa muziki wa benga wa jamii ya Wakamba hutumia mikakati ya kimtindo kama vile ugawaji wa beti, uradidi, urudiaji, tamathali za usemi na aina anui za sentensi kuwasilisha ujumbe. Utafiti huu ni muhimu katika kuufanya muziki wa benga wa jamii ya Wakamba kutambulika katika nyanja za utafiti wa kielimu wa fasihi na lugha kama kategoria ya nyimbo za kitamaduni. Utachangia taaluma ya isimu na mawasiliano kwa kuangazia baadhi ya teuzi za kiisimu zinazofanywa na wasanii
Upakuaji
Marejeleo
Anudo, C. N. A., & Awuor, Q. E. (2018). Music the loaded weapon: War metaphors & ethnicity in Kenyan songs. Journal of Language, Technology & Entrepreneurship in Africa, 9(1), 29-68.
Butler, P. G. (2004). Out of style: A retrospective and prospective look at style in composition theory and practice. Syracuse University.
Campbell, C. A. (1983). Nyimbo za Kiswahili: A socio-ethnomusicological study of a Swahili poetic form (Doctoral dissertation, University of Nairobi,).
Chilala, C. H. K. (2018). A Poetic Analysis of the Lyrics of Contemporary Zambian Popular Music: The Case of General Kanene, Petersen Zagaze and Chef 187. Multidisciplinary Journal of Language and Social Sciences Education, 1(1), 65-101.
Doyle, S. (2017). A review of Millie Taylor’s musical theater, entertainment and realism. Critical Voices: The University of Guelph Book Review Project, 3(3), 22-30.
Enon, J. C. (1998). Educational research, statistics and measurement. Kampala: Makerere University.
Hughes, G. (2015). An encyclopedia of swearing: The social history of oaths, profanity, foul language, and ethnic slurs in the English-speaking world. Routledge.
Jakobson, R. (1960). Closing statement: Linguistics and poetics. Style in language, 350(377), 570-579.
Kenyan History Team. (2025, January 2). The rhythm of Kenya: How youth drive the evolution of popular music. Kenyan History. https://kenyanhistory.com/2025/01/02/a-historical-overview-of-kenyas-music/
Kithome, C. K. (2012). Vernacular radio and traditional music practices in Kenya: case study: Kamba radio of the Kamba community (Doctoral dissertation, University of Nairobi, Kenya).
Kombo, D. K na Tromp, D.L. A (2006). Proposal and Thesis Writing: An Introduction. Nairobi: Pauline Publications Africa.
Kothari, C. (2017). Research methodology methods and techniques by CR Kothari. Published by New Age International (P) Ltd., Publishers, 91.
Leech, G. N. (1969). A Linguistic Guide to English Poetry (English Language Series). Perason Professional Education, USA: Longman Publishers
Muathe, H. M. (2012). A Relevance Theoretical Analysis of the Communicative Effect in Selected Contemporary Kikamba Gospel Music (Doctoral dissertation).
Muema, A. K. (2019). The Linguistic Devices of Euphemism in Kamba: a Case of Kamba Benga Music (Doctoral dissertation, University of Nairobi). http://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/109445
Mulokozi, M. M. (1989). English versus Kiswahili in Tanzania secondary education. Journal of linguistics and language in Education, 4(2), 116.
Naseem, A., & Talaat, M. (2021). Examining the Functions of Graphological Deviation in Redeeming Love by Francine Rivers. Global Language Review, VI(IV), 112-125. https://doi.org/10.31703/glr.2021(VI-IV).11
Nduku, D. C. (2020). Construction of Masculinity in Kenyan Popular Music: A Close Analysis of Selected Kamba Popular Performances (Doctoral dissertation, University of Nairobi).
Ngungi, D. T., & Mwihia, M. N. (2022). A critical analysis of stylo-thematic and performance of Kamba traditional and modern secular songs. International Research Journal of Social Sciences, Education and Humanities, 3(3), 96–110. https://www.irjp.org/index.php/IRJSEH/article/view/96
Njogu, K., & Chimerah, R. M. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na mbinu (Vol. 1). Jomo Kenyatta Foundation.
Okal, B. O. (2020). A Psycho-Realist Analysis of Gabriel Omolo's 'Lunch Time' Music. EAS Journal of Humanities and Cultural Studies July. https://doi.org/10.36349/EASJHCS.2020.V02I04.03
Omolo, H. O. (2014). A lexical pragmatic approach to Ohangla music: A case of metaphors (Doctoral dissertation, University of Nairobi).
Ooko, A. (2008). A Pragnatic Analysis of Man Talk in Kenyan Print Media. University of Nairobi. Unpublished M.A. Thesis.
Red Bull Music Academy. (2019). Red Bull Music Academy Daily. Retrieved June 6, 2025, from https://daily.redbullmusicacademy.com
Wambua, S. (2001). Mtindo na matumizi ya Lugha katika nyimbo za Kakai Kilonzo. Tasnifu ya MA Chuo Kikuu Cha Kenyatta. Haijachapishwa.
Wanyama, J. K., & Wandera, P. S. (2018). Ubandikaji Majina na Majumlishi Memeto kama Mikakati ya Propaganda Katika Mdahalo wa Urais wa Kenya 2013.
Yule G. (2022). The study of language. Cambridge University Press.
Copyright (c) 2025 Carolyne Muthini Mutuku, John Khaisie Wanyama, PhD, Timothy Kinoti M’ngaruthi, PhD

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.