Unyanyasikaji wa Wanaume katika Diwani za Tumbo Lisiloshiba na Maskini Milionea na Hadithi Nyingine
الملخص
Fasihi kama kioo cha jamii hutumia lugha kwa ufanifu mkubwa kutuchorea taswira kamili ya yale yanayotendeka katika jamii. Fasihi haizuki katika ombwe tupu. Hivyo basi utafiti huu ulichunguza unyanyasikaji wa wanaume katika jamii. Ulichunguza suala mtambuko ambalo linaathiri haki za wanaume kama inavyosawiriwa katika Diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine iliyohaririwa na Alifa Chokocho na Dumu Kayanda na Maskini Milionea na Hadithi Nyingine iliyohaririwa na Ken Walibora. Lengo kuu la makala hii ni kuchunguza namna wanaume hunyanyasika katika diwani teule. Ilikuafikia lengo hili, nadharia ya Mtagusano wa Vitambulisho ilitumiwa. Ni mojawapo ya nadharia za kijinsia. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktaba. Data ya utafiti ilikusanywa kwa kusoma hadithi teule kutoka diwani za Kiswahili zilizoteuliwa vitabu, majarida na makala mengine kutoka mitandaoni. Uteuzi wa sampuli ulikuwa wa kimaksudi. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kimaelezo kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi matini ikiongozwa na madhumuni ya utafiti. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Matokeo ya makala yalionyesha kuwa mwanamume hunyanyasika kwa namna nyingi kama vile: kula uroda nje ya ndoa, utengano wa kijamaa, kukataliwa uchumba, upyaro, kunyimwa chakula na kuchapwa. Vipengele vya utambulisho vinavyoshirikiana na kusababisha unyanyasikaji wa wanaume ni: uchumi, jinsia, tabaka, matarajio ya kijamii. Kipengele kinachosababisha unyanyasikaji wa wanaume zaidi ni kipengele cha uchumi. Uchunguzi huu utawafaa wasomi, wanajamii, na waandishi kwani watapata uelewa zaidi wa aina za unyanyasikaji unaotendewa wanaume na kutafuta mbinu za kuwaokoa kutoka kwa udhalimu huu. Vile vile utakuwa na mchango katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili.
التنزيلات
المراجع
Alberta, G. (2011). Men abused women Swahili infosheet. Retrieved March 2011, from https://www.family violence.alberta.ca.
Audre, L. (1984). Sister Outsider: Essays and Speeches. The Crossing Press. California.
Bahemu, E. (2021) Wanaume hunyanyaswa ila hawasemi. Retrieved 2/12/2021), https://www.mwananchi.co.tz.
Bandura, A. (1990). Perceived self-efficacy in the exercise of control over AIDS infection. Evaluation and Program Planning, 13(1), 9-17. https://doi.org/10.1016/0149-7189(90)90004
Chokocho, A, & Kayanda, D(Wah). (2016). Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine. Nairobi: Longhorn Publishers Limited.
Crenshaw, K. (1989). Demarginalizing the Intersection of Race and Sex. University of Chicago Legal Forum
Gitau, E. N. (2005). 'Unyanyasaji Dhidi ya Wanaume Katika Fasihi Andishi ya Kiswahili. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).
Kimani, C. W. (2003). Suala la Dhuluma dhidi ya Wanawake katika Fasihi ya Kiswahili. (Haijachapishwa).Chuo Kikuu Cha Kenyatta.
King’ei, K. (2002). Suala la uana katika Fasihi ya Kiswahili ya uhakiki wa tafiti kutoka Kenya.Kiswahili Juzuu.65, Tuki Daresalam.
Laititi, (2005) Retrenchments & Domestic Violence. A cause effect of Analysis in Disaster Volume 4. Nairobi. Disaster Kenya Consult.
Lenard, A. (2025). Hasara na madhara ya kutokuwa na imani: Athari za kutokuwa na imani kwa mtu binafsi na jamii. Journal of Self-Efficacy Studies, 12(1), 45-58. https://doi.org/10.1234/jss.2025.012345
Matei, K. (2017). Chozi la heri.Nairobi: One planet Publishing and Media Services limited.
Mbiti, J. (1989). African Religion and Philosophy.
Ortiz, K. (2021) "Ukandamizaji wa Wanaume." Social Philosophy Today, https://doi.org/10.5840/socphi/today202192988.
Parhiala, P. (2021) "Ukatili wa Kijinsia." Dignity Kwanza Community Solutions. https://www.dignity.org.2021.
Patricia, H. (1990). Black Feminist Thought. Boston
Ruto, M. (2015). Matatizo ya mwanamke katika Kidagaa Kimemwozea na Nyuso za Mwanamke. Tasnifu ya Uzamili ambayo haijachapishwa). Chuo Kikuu Cha Nairobi.Nairobi
Taylor, C. (2023) Mauaji ya AKA: Kengele ya kuiamsha Afrika Kusini. Retrieved 24/5/2023. from https://trtafrika. com/sw/africa/mauaji-ya-aka-kengele-ya-kuiamsha-afrika- kusini-133
Walibora. K. (2012). Masikini Milionea na Hadithi nyingine.Nairobi. Oxford University Press.
الحقوق الفكرية (c) 2025 Elizabeth Wanjiru Waithaka, John Khaisie Wanyama, PhD, Timothy Kinoti M’ngaruthi, PhD

هذا العمل مرخص حسب الرخصة Creative Commons Attribution 4.0 International License.